-Mwinjilisti Benadertha Magumba |
Kuiitii sauti ya Mungu na maagizo yake ikiwa ni pamoja na
kuyatumikia mungu hufanya jambo katika maisha ya mkristo na baraka zake humpandishwa
katika viwango vya juu kama neno linavyosema uliangalia neno lake na
kulitimiza.
Hayo yameelezwa na mwinjilisti Bernadetha Josephat Magumba wa
kanisa la Holy Ghost Revival Ministry, lililopo miti ya nyerere jijini Mwanza,
katika ibada iliyofanyika kanisani hapo hivi karibuni.
Amesema ili Mungu aweze kufanya jambo katika maisha ya mwamini ni
lazima aweze kujua Mungu anataka nini na hapendi mambo gani ambayo ni chukizo
kwake na kuongeza kuwa wakristo wengi wamekuwa wakitaka baraka lakini
hawajataka kujitenga mbali na dhambi jambo ambalo ni chukizo mbele za Mungu na
hakuna baraka inayokuja bila kufanya ushirika na Mungu katika roho na kweli.
Aidha mwinjilisti magumba amewataka wakristo kuacha tabia ya mazoea
katika kumuomba mungu huku wengine wakizidi kuendekeza mila za koo zao jambo
ambalo halimpi Mungu utukufu na kwa kufanya hivyo ni kuendelea kuitumikia
miungu na kumfanya Mungu kuwa kinyume nao.
-Mwinjilisti Benadertha akiwa na mmewe mchungaji kiongozi wa kanisa la Holly Ghost Revival Ministry Josephat Magumba |
No comments:
Post a Comment