Kila kukicha dunia haiishi maajabu,mengine yakiwa ni yale
ambayo yako kinyume kabisa na mapenzi ya mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na
dunia.
Afrika kusini imeingia kwenye orodha ya ncchi za maajabu na
vituko baada ya taarifa mpya za hivi karibuni kubainisha kuwa hivi karibuni vyuo
vikuu nchini humo viitaanza kufundisha kisha kutunuku shahada(degree)ya masuala
ya uchawi na ushirikina.
Waziri wa elimu ya juu na mafuzo wa nchini Afrika Kusini Blade
Nzimande ametangaza mpango huo wa kuingiza masuala ya uchawi na ushirikina
katika mtaala mpya wa masomo wa mwaka 2018 ili kuwapa nafasi ya kujifunza kwa
undani masuala hayo wanafunzi ambao watakuwa tayari katika vyuo vikuu vya
nchini humo.
Waziri huyo ametangaza nia hiyo mbele ya wanafuzi katika
mkutano wawakilishi wa umoja wa wanafunzi wa taifa hilo ambapo amesema lengo la kozi hiyo ni
kuwapa ujuzi wa kutosha wanafunzi wanaovutiwa na masuala ya ushirikina kwa
ustawi wa jamii.
“Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wachawi,kama vile jinsi
wanavyopaa katika ungo.Hebu vuta picha kama tutajifunza ujuzi huo itamaliza
kabisa tatizo la msongamano wa magari barabarani na kila mtu atapanda tu ungo
na kupaa,inamaanisha pia kwamba hatutaingiza tena nchini mafuta ya magari”.Alisema
Blade
Bwn:Blade aliongeza kuwa anatoa wito kwa wachawi wote wenye
ujuzi kufika ofisini kwake ili wafanyiwe usahili na wale watakaopita waajiliwa
kama walimu wa vyuo vikuu(lectures).
Aliongeza kuwa mwaliko huo pia unawahusu wachawi wote
waliyoko nje ya Afrika kusini ambapo ameahidi kuwapa kibali cha kudumu cha
wakazi.
Kutokana na tangazo hilo,wanafunzi wawakilishi katika mkutano huo walifadhahishwa na matamshi hayo kwani wengi wao walienda katika mkutano huo wakitegemea waziri huyo angetangaza ongezeko la 0% ya ada kwa mwaka ujao,ambapo katika hali ya kuoneshwa kuchukia walimzomea waziri huyo na kumponda kwa chupa za maji.
Maombi ya kujiunga na kozi ya uchawi
na ushirikina kwa wanafunzi ambao wamevutiwa nayo inasemekana kufungwa September
30 usiku wa manane na kutakuwa na nafasi
za kazi kwa wachawi wapatao 109.
No comments:
Post a Comment