
Video ya Amenifanyia Amani ya Mwimbaji Paul Clement imefungua mlango mwingine wa muziki wa Injili kimataifa baada ya kuchezwa kwenye kituo kikubwa cha Televisheni cha kimataifa cha MTV Base.
Hili sio jambo la mchezo,kwa ukubwa wa kituo hicho cha Tv inamaanisha kuwa video hiyo ya mkali wa Gospo Paul Clement iliyoongozwa na Director Einxer ipo katika viwango vya ubora wa kimataifa na pia mwimbaji huyo yupo tayari kuingia kwenye orodha ya waimbaji wa kimataifa.
Katika harakati za kutaka kujua zaidi kuhusiana na njia ambazo mwimbaji Paul Clement amepita kufikia hatua hiyo tumeongea na meneja wa Paul Clement,Gee Maarufu ili atugemee siri kidogo.
Kwa upande wake meneja wa Paul ameeleza kuwa siri kubwa ni kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu na pia kuna taratibu za kufuata ili video ichezwe kwenye channel na kuongeza kuwa hata wao walituma video hiyo wiki tatu kabla na baada ya kufanyiwa Quality Chek ndipo ikachezwa,
“kikubwa ni video kuwa katika ubora mkubwa. kuna taratibu za kufuata ili iweze kuchezwa mtv. ingawa tuliipeleka wiki tatu nyuma ikaazwa kukaguliwa kama QC (quality check) then wakatujibu imepita kwenye ubora wa viwango vyao na wataanza kuicheza” alisema Meneja wa Paul na kuwatakamwaimbaji wawekeze kwenye ubora na promotion.
Meneja huyo pia ameweka wazi kuwa hawataishia hapo bali watazidi kufungua milango mingine ya kimataifa ambapo kwa sasa yeye na Paul Clement wako nchini Kenya wakifanya ziara mbalimbali kwenye vyombo vya habari.
Je! umeshaitazama video hiyo? kama bado itazame sasa
Source:GospoMedia
No comments:
Post a Comment