Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mwanza walihudhuria semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Kassa charity kisesa Mwanza,ambapo waliweza kupata masomo mbalimbali kutoka kwa watangazaji wa vipindi vya injili vya redio za Jijini Mwanza.
Watangazaji hao katika umoja wao waliamua kuandaa semina hiyo wakishirikiana na Promover Manegement kwaajili ya kuzungumza na waimbaji wa muziki wa injili ikiwa ni sambamba na kupata maoni ya jinsi ya kuendeleza huduma hiyo.
Katika semina hiyo waimbaji hao walitoa changamoto zinazowakabili pamoja na maoni yao kwa watangazaji ambao kwa upande wao walitoa masomo mbalimbali ya kuwajenga waimbaji.
Baadhi ya waimbaji waliohudhulia semina hiyo walisema wamepokea vitu vingi ambavyo wanaamina vitawapandisha kwa hatua kubwa kimuziki ambapo pia walisema wanahitaji semina nyinginezo kama hizo ili wazidi kukua katika sanaa.
Kwa upande wao baadhi ya watangazaji waliotoa masomo katika semina hiyo,wakizungumza na Promover.com wamesema wamepata maoni mengi kutoka kwa waimbaji ambao wengi wamependekeza kuanyika tena semina kama hiyo.
Habari za ndani kutoka kwa kamati ya maandalizi ya semina hiyo ni kwamba semina nyingine kubwa kwa waimbaji itafanyika mapema mwakani.
Tazama baadhi ya picha katika semina hiyo:
No comments:
Post a Comment