Jumamosi ya tar 31/12/2016 ndo ilikuwa siku ya mkesha
kwaajili ya kuupokea mwaka mpya wa 2017 ambapo katika kanisa la TFE kwaneema
mkesha huo ulfana sana kwani wakazi wengi wa jiji la Mwanza walijitokeza
kupokea Baraka za Mwaka mpya.
Mkesha huo ulioongozwa na mchungaji kiogozi wa kanisa
la TFE Kwaneema Mch Philipo Stanslaus kwa ushirikiano na Mchungaji Paul Chaba.
Wakristo Nchini Wametakiwa Kujichunguza Na Kujiuliza
Maswali Mawili Katika Maisha Yao Pindi Mungu Akiwachukua Na Kuwauliza Walifanya
Nini Duniani Juu Ya Yesu Na Pia Walifanya Nini Juu Ya Kutumia Karama Zao Katika
Kumtumikia Mungu Na Maisha Yao Kwa Ujumla.
Kauli Hiyo Ilitolewa Na Askofu Mkuu Wa Kanisa La
Tanzania Field Evangelism T.F.E Kwaneema Askofu Augastine Mpemba Katika Mkesha
Wa Kufunga Mwaka 2016 Na Kuupokea Mwaka 2017 Katika Kanisa La T.F.E Kwaneema
Lililopo Kona Ya Msumbiji Jijini Mwanza.
Alisema Katika Maisha Ya Ukristo Ni Lazima Kila Mkristo
Ajue Kuwa Kuna Siku Ambayo Utasimama Mbele Za Mungu Na Kuweza Kumwambia Habari
Zako Jinsi Ambavyo Uliishi Katika Dunia Hii Na Pindi Ushindwapo Kujibu Maswali
Ya Mungu Utapokea Matokeo Ya Majibu Yako.
Pia Skofu Mpemba Alingeza Kuwa Katika Mwaka 2017 Ni
Mwaka Wa Kukaza Mwendo Haijalishi Hata Kama Kuna Magumu Mangapi Ambayo Watu
Wanapita Ila Ni Mwaka Wa Kukaza Mwendo Kwa Ajili Ya Kufanikiwa Zaidi.
No comments:
Post a Comment