Chumba kidogo kinachofunika kaburi
ambako inaaminika Yesu Kristo alizikwa kimefunguliwa rasmi tena baada ya
kufanyiwa ukarabati kwa miezi tisa.
Aidha, kilikuwa limebadilika rangi na kuwa karibu rangi nyeusi kutokana na masizi ya mishumaa mingi ambayo huwashwa eneo hilo.
Mzozo kati ya madhehebu matatu ambayo kwa pamoja husimamia kanisa hilo - Kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, Kanisa la Kiarmenia na Kanisa Katoliki la Kirumi - ulichelewesha ukarabati huo kwa miongo mingi.
Antonia Moropoulou, aliyesimamia ukarabati, amesema chumba hicho sasa kimepata tena rangi yake asili inayokaribia hudhurungi.
Chumba hicho kilifanyiwa ukarabati mara ya mwisho mwaka 1810.
No comments:
Post a Comment