Pages
▼
29 September 2017
PICHA ZA KANISA LA MITI NA NYUMBA YA TOPE YA MCHUNGAJI ZAZUA GUMZO MTANDAONI,SHIKAMOO YESU AZITOLEA UFAFANUZI
Injili na ihubiriwe mjini na vijijini,hivyo ndivyo unaweza kusema kuelezea jambo hili ambapo picha za kanisa na nyumba ya mchungaji wa kijijini zimezua gumzo sana mtandaoni.
Gumzo kuhusu picha hizo ni kutokana na nyumba ya ibada yaani kanisa pamoja na nyumba ya mchungaji ambazo ni za miti na matope kabisa,huku injili ikiendelea kama kawaida.
Picha hizo zimesambazwa na muimbaji wa nyimbo za injili kutoka mkoani Mbeya anayeitwa Mathias Mwanyamaki maarufu kwa jina la 'Shikamoo Yesu' ambapo katika picha hizo anaonekana akiwa mazingira tofauti toauti huko Morogoro vijijini alikokwenda kufanya huduma ya uimbaji.
Kupitia mitandao ya kijamii wengi wameonekana kuguswa na picha hizo wakitaka kufamfahamu mchungaji pamoja na kanisa hilo huku wengine wakiomba namba ya simu ya mchungaji ili waweze kuchangia pesa kuweza kumuinua mchungaji huyo.
Akizungunza na promovertz.com Mathias alisema picha hizo ilikuwa ni katika kijiji cha Mkambarani kinachopatikana Morogoro vijijini na kanisa hilo ni la EAGT chini yake mchungaji Filimon.
Mathias alisema alikuwa na wakati mzuri sana katika kijiji hicho ambapo alipata mapokezi makubwa na kukamilisha huduma yake salama.Kwa sasa Mathias yuko mkoani Dar es salaam ikiwa ni siku chache tu tangu atoke mkoani Mtwara ambako pote ameenda kwaajili ya huduma hiyo ya uimbaji.
Karibu sasa usikilize wimbo maarufu kutoka kwake Mathias Mwanyamaki wimbo unaoitwa 'Shikamoo Yesu' Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Mathias kwa simu namba:0767910912
No comments:
Post a Comment