Pages

30 September 2017

SEHEMU YA 2 YA MKASA WA MAMA WA KAMBO,USHUHUDA WAKE MANONGA CLASSIC

 
Karibu katika sehemu ya pili ya ushuhuda wake Manonga Classic ambaye kupitia ukurasa wake wa Facebook aliamua kuanika historia ya maisha yake ushuhuda alioupa jina la 'Mkasa wa Mama wa Kambo'.

Tuendelee......
 


HUYU NDIE MDOGO WA MIMI ANAENIFATIA ALIYEPEWA MASHARTI YA KUTUMIA KIKOMBE CHEKUNDU WAKATI WA KUNYWA JUICE.

BAADA YA KUMJIBU MAMA WA KAMBO KWAMBA NIKO SAWA NA NIKO VIZURI TU GHAFLA SURA YAKE IKAWA KAMA IMEBADILIKA KWA KUONA KILE ALICHOKITARAJIA HAKIKUFANIKIWA.

ZILIPITA SIKU KADHAA NIKAMUELEZA BABA JUU YA TUKIO LILE LILILOTOKEA BABA AKASEMA NITALISHUGHULIKIA JAMBO HILI SIKU MOJA NIKIWA NIMELALA USIKU NILISIKIA BABA AKIFOKA SANA JUU YA MAMA KWA KILE TULICHOMUELEZA BAADA YA KUTOKEA MARUMBANO HAYO IKAWA TUKIMSALIMIA MAMA WA KAMBO HAITIKII TULIVUMILIA NA HALI HIYO KWA KUTUONA MAADUI WAKUBWA SANA KWAKE.

SIKU ZILIENDA MIAKA IKASONGA MAISHA YAKAENDELEA.
MAISHA YALIKUJA KUBADILIKA NAKUWA MACHUNGU NA MAGUMU SANA KWETU PALE BABA ALIPONUNUA ENEO LA KUJENGA NDIPO SHETANI ALIPOANZA KUJIDHIRISHA WAZIWAZI BAADA YA KUTUKOSA KATIKA MITEGO YAKE YOTE ALIGEUZIA UPANDE WA BABA CHUKI ILITAWALA JUU YANGU HASIRA ILIPAMBA MOTO JUU YANGU NILIJIKUTA NAFOWEKA PASIPOKUJUA MAKOSA YANGU KUMBE KILE KITENDO KILIKUWA KINAMFURAHISHA SANA MAMA WA KAMBO MAISHA YA KUSOMA YAKAWA MAGUMU SANA MAMA WA KAMBO AKAINUA CHUKI JUU YA MDOGO WANGU KILA ANACHOKIFANYA KWAKE HAKIKO SAWA UMBALI WA SHULE ULIKUWA NIMREFU SANA NAAMKA SAA KUMI NAFATA MAJI UMBALI MREFU NARUDI NIJIANDAE KWENDA SHULE NIMEISHACHELEWA NIKIFIKA SHULE SAA TATU MASOMO MENGINE YAMEPITA NAAMBULIA KUCHAPWA KWA UCHELEWAJI.

ILIKUWA NISHIDA ILIKUWA NITABU ILIKUWA NIMAUMIVU
SAA KUMI NA MBILI UKIRUDI KUTOKA SHULE UNAKUTA CHAKULA HUJAACHIWA INABIDI UFATE MAJI KWA AJILI YA MATUMIZI YA USIKU MUDA WA KUJISOMEA ULIKOSA KABISA ILIFIKIA HATUA BABA HAJALI WALA HATHAMINI KABISA KINACHOHUSU MAISHA YA SHULE AMA MAISHA YA KIBINADAMU
SIKU MOJA NARUDI KUTOKA SHULE NAMKUTA BABA AMERUDI KUTOKA KAZINI AMBAPO ILIKUWA SI KAWAIDA YAKE NA AMELALA KITANDANI NIKAMUULIZA BABA MBONA LEO MAPEMA ALINIJIBU KWA HASIRA SANA AMBAPO NILIJISIKIA VIBAYA SANA.

KADRI SIKU ZILIVYOKUWA ZIKIENDA HALI YA MZEE ILIZIDI KUBADILIKA GHAFLA MGUU WA MZEE WANGU WA KUSHOTO ULIANZA KUWA MFUPI NA KUWA MWEMBAMBA KABISA MADONDA MAJIBU NGOZI KUBADILIKA NA MATESO KUWA MAKUBWA KWA BABA YANGU MACHOZI YALINITOKA KUONA HALI YA BABA IKO VILE.

ILIFIKIA HATUA BABA YANGU AKAWA MLEMAVU WA MIGUU AKITEMBEA ANACHECHEMEA MOYO ULIUMA MACHOZI YALINITOKA KWANI MFUMO WA MAISHA YA BABA YANGU YALIBADILIKA.

PAMOJA NA HALI YAKE KUWA VILE LAKINI HASIRA YA BABA ILITAWALA SANA JUU YANGU KUMBE HALI ILE ILIZIDI KUMPA FURAHA MAMA WA KAMBO CHAKULA ILIFIKIA IKAWA SHIDA CHAI NA VYAKULA VINGINE VILIVYO VIZURI TULIVISIKIA KWA MAJIRANI MLO WA ASUBUHI ULIKUWA NI UJI USIO NA SUKARI JANUARY HADI DECEMBER ILA KWA MTOTO WAKE SUKARI ILIKUWA HAIKOSI CHAKULA CHA MCHANA NA USIKU ILIKUWA NI UGALI MCHICHA MWANZO WA MWAKA HADI MWISHO WA MWAKA.SIKU MOJA NIKIWA CHUMBANI KWANGU NIKIJARIBU KUJISOMEA GHAFLA DILISHANI NILIONA MKONO WA MTU UKINIITA PASIPO KUONA SURA YA MTU ANAENIITA NILIPIGA KELELE BABA AKASHITUKA NA KUTOKA NJE KUONA KIMETOKEA NINI ALIZUNGUKA NYUMBA ZIMA HAKUNA KITU KUMBE YULE MAMA ALIJUA KINACHOENDELEA NILIMUOMBA MDOGO WANGU ANIPE KAMPANI USIKU ULE AKALALA KWENYE KOCHI MIMI NIKALALA KITANDANI.

HALI YA BABA ILIZIDI KUBADILIKA SANA IKAFIKIA HATUA AKAWA KAMA ANAPANDISHA MAPEPO NAKUANZA KUPIGA KELELE OVYO AKILI ILINITUMA NISHIKE BIBLIA NIMUOMBEE NIKAANZA KUKEMEA ILIHALI SIKUWA NIMEOKOKA BALI NILIJUA NIKIFANYA VILE NITAMSAIDIA BABAANGU AFYA YA MZEE ILIZOROTA MAISHA SASA YAKAZIDI KUWA YATABU IKAFIKIA HATUA SASA BABA AKASEMA SISI NA MAMA YETU MZAZI NDIO TUNAOMLOGA BABA BAADA YA KUAMBIWA NA MAMA WA KAMBO KWAMBA WANAO NA MAMA YAO WANATAKA WAKUUE ILI WARITHI ENEO.

SIKU MOJA BABA ALIAMKA NAKUANZA KUTOA MANENO AMBAYO SIKUYAELEWA AKISEMA HAKUNA MTU ATAKAECHUKUA MALI ZANGU WALA HAKUNA ATAKARITHI MALI ZANGU MKATAFUTE ZENU NA MAMA YENU MOYO ULIUMA NILILIA KUSIKIA MANENO YALE NILIJIPA MOYO NA UVUMILIVU MWINGI NIKIJUA SIKU MOJA YATAKWISHA.

BABA YANGU ALIANZA KUTEMBEZWA KWA WAGANGA WA KILA AINA WAGANGA WALIPISHANA NYUMBANI KAMA KWAO MAISHA YALIENDELEA HIVYO. SIKU MOJA NILIAMKA SAA KUMI NA MOJA KUFATA MAJI KISIMANI KWA BAISKELI UMBALI KAMA MBEZI MWISHO HADI KARIAKOO NILIPOKUJA KURUDI MAJIRA YA SAA NNE NDIPO NILIPOKUTA UJUMBE KWA MDOGO WANGU AMBAO BABA ALIUACHA UKISEMA TUISHI KWA AMANI NA TUPENDANE KUMBE BABA YANGU ALIPANGA SAFARI YA KUELEKEA KWAO PASIPO MIMI KUNIAMBIA HADI PALE TULIPOKUJA KUPATA TAARIFA YA KIFO CHA BABA YANGU.

...UNATAKA KUJUA NINI KILIENDELEA......Usikose sehemu ya 3 

No comments:

Post a Comment