Promover
Management Entertainment Wanakuletea ‘TUNGO ZA INJILI’.
Ni semina elekezi kwa waimbaji wa nyimbo za injili na
wadau wa muziki wa injili Mwanza.Masomo yatafundishwa na wawezeshaji mbalimbali
wakiwemo watangazaji wa redio na tv,wachungaji,waandaji wa muziki na viongozi
wa serikali.
Masomo yatakayofundishwa ni pamoja na:
1.Mwimbaji na Maadili na nidhamu katika jamii(kujitambua)
2.Jinsi ya kujisajili Basata
3.Jinsi ya kusajili kazi Cosota(haki miliki ya producer
na mwimbaji)
4.Mifumo ya usambazaji wa kazi za waimbaji(cd/dvd)
5.Elimu ya mlipa kodi kwa mwimbaji kupitia stika za
tra(cd stamp)
6.Jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kukuza muziki.
Pia mijadala ya kina itafanyika kuhusu changamoto ya
muziki wa injili,jinsi ya kutatua na namna bora ya kukuza muziki huo Tanzania
na Duniani.
Semina hiyo itafanyika siku ya jumamosi tar 24/2/2018
katika hoteli ya JB Belmout Fairmount (NNSF Mafao House Mwanza) kuanzia saa 4
asubuhi hadi saa 12 jioni.
Waimbaji ambao wanapenda kushiriki katika semina hii
watatakiwa kuchangia Tsh.10,000/= ambayo ni kwaajili ya chakula katika semina
hiyo pesa hiyo itumwe kwenye simu namba:0755255844 au kununua tiketi kwenye
kituo cha Jb Belmount Fairmount Hotel kwa Tsh 10,000/=.
Mwisho wa kuthibitisha ushiriki kwa kutuma michango ni tar
22/2/2018.
Hii ni semina ya pili elekezi kwa waimbaji wa muziki wa
injili jijini Mwanza kuandaliwa na Promover ambapo mara hii wameiboresha Zaidi na
inategemewa kuwa na washiriki wengi Zaidi.
No comments:
Post a Comment