Kiongozi wa kanisa Katoliki
Papa Francis anahitimisha ziara yake ya kihistoria katika Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE) na anatarajia kuongoza misa waumini wa kanisa Katoliki nchini
humo.
Papa Francis amepongeza Umoja
wa Falme za Kiarabu kwa kutokuwa na ubaguzi wa kidini na kusema kuwa nchi hiyo
inatakiwa kuwa mfano kwa mataifa mengine yenye ubaguzi wa kidini.
Pia amekaribisha juhudi za
Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kuwapa ajira wahamiaji ambao wengi wao ni kutoka
Ufilipino na India.
Umoja wa Falme za Kiarabu una
wakazi zaidi ya 85% ya wahamiaji. Raia kutoka nchi za Asia ni asilimia 65 ya
wakaazi wa nchi hiyo na wameajiriwa katika sekta zote, kuanzia ujenzi hadi
katika hoteli.
Takribani Wakatoliki milioni
moja wanaishi katika Umoja wa Falme za Kiarabu, sawa na mkaazi mmoja kati ya
kumi.
Umoja wa Falme za Kiarabu una
makanisa nane ya Katoliki,ambayo ni idadi kubwa ya makanisa Katoliki katika
kanda hiyo.
Ziara hiyo ya kiongozi wa kanisa Katoliki duniani ni ya kwanza
kuwahi kufanywa na kiongozi wa kanisa hilo kwenye rasi ya Uarabuni.
Lengo ni kufungua ukurasa mpya katika uhusiano baina ya
wakristo na Waislamu.
Mrithi wa mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zayed Al
Nahyan alimpokea Papa Francis kwenye uwanja wa ndege akiwa na tabasamu huku
akiongozana na mawaziri wake.
Imam mkuu wa msikiti maarufu wa Al-Azhar wa nchini Misri, Ahmed
el Tayeba pia alikuwapo uwanja wa ndege kumlaki Baba Mtakatifu.
Papa Francis na imam el Tayeb watahutubia kwenye
mkutano utakaohudhuriwa na wawakilishi wa dini zote.
Waumini wapatao 135,000
wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo ya hadharani.
No comments:
Post a Comment