Waimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Beatrice Mwaipaja,Angel Benard,Christina Shusho naye Bonny Mwaitege,ni miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili wanaoshindana katika Tuzo za injili Afrika Mashariki zinazoitwa East Africa Gospel Awards(EAGA)
Watanzania wengine ni Calvary G Band,Mbagwa
Hassan,Innocent Mujwahuki,Victoria Martin,Makeke.
Njia ya kuwapigia kura watanzania hawa kwenye tuzo
hizo zitakazofanyika mwezi wa 12 ni kwanza kabisa kuhakikisha unayo barua pepe(email)
Kama una email utaiweka kwenye eneo palipoandikwa
Email Address kisha utaanza kupiga kura kwa chini,zingatia kwamba utatakiwa
kuchagua mshiriki mmoja kwa kila kipengele unachopiga kura na hata vile
vipengele ambavyo havina mshiriki unayemtaka unatakiwa tu kumchagua mmoja
yeyote ili uweze ku submit kura zako.
Karibu sasa upige kura,bonyeza>>PIGA KURA HAPA
No comments:
Post a Comment