Waimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini
Tanzania Beatrice Mwaipaja,Angel Benard,Christina Shusho naye Bonny Mwaitege,ni
miongoni mwa waimbaji wa nyimbo za injili wanaoshindana katika Tuzo za injili
Afrika Mashariki zinazoitwa East Africa Gospel Awards(EAGA)
Tuzo hizo zinazoandaliwa nchini Kenya zinajumuisha
waimbaji na wadau mbalimbali wa muziki wa ijili kutoka nchi za Afrika Mashariki
ambapo utoaji wa tuzo hizo unategemewa kufanyika tarehe 11 DEC nchini Kenya.
Beatrice Mwaipaja anayetamba na wimbo wa Mungu
umenihurumia,amechaguliwa kushiriki kwenye vipengele viwili Wimbo bora kuabudu
na video bora ya mwaka kwa wimbo wake wa Mungu umenihurumia.
Kwa upande wake Christina Shusho yeye yuko kwenye kipengele kimoja cha Mwimbaji bora wa kike wa mwaka,ambapo anashindana na waimbaji wengine Mercy Masika(Kenya) Tonzi(Rwanda) Janet Otieno(Kenya) Judith Babirye(Uganda) na Gambi Kamanzi(Rwanda).

Bonny Mwaitege yeye kachaguliwa kushindana katika kipengele cha Mwimbaji bora wa kiume wa mwaka,ambapo anashindanishwa na waimbaji wengine Kim(Rwanda) Isreal Mbonyi(Rwanda) Pastor Bugembe(Uganda) Bahati(Kenya) na Piston(Kenya)
Watanzania wengine waliochaguliwa kushindana kwenye tuzo hizo ni pamoja na Calvary G Band kipengele cha Bandi bora ya mwaka.
Innocent Mujwahuki yeye ni kwatika kipengele cha mzalishaji
bora wa muziki(Audio Producer of the year)
Mbagwa Hassan anashindana kwenye kipengele cha mwongozaji bora wa video wa mwaka.
Victoria Martin anashindana kwenye kipengele cha Mlimbwende/Mwanamitindo
wa kike wa mwaka.
Kampuni ya Makeke ya nchini Tanzania inashindana
katika kipengele cha Nembo bora ya Mitindo ya mwaka.
No comments:
Post a Comment