Jiji la Mbeya ni la pili kwa
wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya,Paul Ntinika,jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una
madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.
Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji
David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism
Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka
na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila
kukicha.
Meya huyo ambaye pia ni msimamizi
wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna
ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu,sheria
na misingi ya Mungu.
Amesema madhehebu mengi ya
kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya
awali kutokana na migogoro.
“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo
vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani,
Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa
kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya
huyo.
No comments:
Post a Comment