Siku
tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la
Maombezi (GRC),Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo
akisema anaishi kana kwamba hana jirani.“...Tunaishi
kama majambazi tu,hujui jirani yako ni nani,” amesema.
Alhamisi iliyopita,mitandao ya kijamii ilikuwa na picha
zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani yake lakini
mchungaji huyo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo ambalo lilisambaa baada ya
mwandishi wa habari,Happiness Katabazi aliyeshuhudia mzozo huo,kuandika kwa
kirefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.
Picha ya video iliyosambaa mitandaoni ilimuonyesha mtu anayedaiwa kuwa ni mchungaji Lusekelo akijibizana na sauti ya mwanamke, ambaye haonekani,huku gari la rangi nyeusi aina ya Toyota Landcruiser likiwa limeegeshwa katikati ya barabara ya mtaani na kuzuia mengine kupita.

Lusekelo amesema Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.
Amesema
magazeti wa mitandao ya kijamii hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpandisha
ila Mungu pekee.
Katika
mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili
nyingine za karibuni kanisani kwake,Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia
kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza
kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.
Katika
mahubiri hayo alisema haiogopi jela,bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na
wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo,kwani viongozi wa
dini wamekula kiapo hadi kufa.
Aidha,alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana,alidai kuwa matusi
yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize
yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.
Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.
Hata hivyo,aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.
Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo,alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.
“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza
magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza
maana ni kibarabara...washenzi
wakubwa wanaandika tu,halafu
wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na
wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi.Kila mmoja anatumia gari
lake,” alieleza Mzee wa Upako.
“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja
kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa.Wakati mnajitokeza
hapa mbele (kutoa sadaka),alipita mama mmoja amebeba mtoto,nilimwombea mwaka
jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto,sasa mbona magazeti
yasiandike habari hizo?”
“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’
(ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani, matatani babu yako.”
“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme,nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema,baada ya mwezi
mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”alisema.
Chanzo: Mwananchi
No comments:
Post a Comment