Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua
wadudu inayoitwa Doom waumini amelaaniwa vikali.
Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook,mchungaji
aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua
waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.
Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa
hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika
kuwasilisha malalamiko.
Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa
anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.
Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa
kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.
Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na
Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly
katika jimbo la Limpopo, anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa
moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini
wa kanisa lake.
'Nguvu za Mungu'
Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".
'Nguvu za Mungu'
Amemueleza mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".
Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na
virusi vya HIV vinavyosababisha.
Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema
kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ''nabii'' huko Limpopo - Lethebo
Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu
ya imani ya kuabudu:
''Tunaona tendo hili kuwa kutia hofu kubwa,na
tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine
yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu''.
''Doom ilitengenezwa kwa ajili ya
kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo, na maelezo
yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa
kufuatwa.''
''Kampuni ya Tiger iko katika
mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo,'' imesema
kampuni ya Tiger.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment