Kiongozi wa kanisa katoliki Papa
Francis amewateua makadinali wapya wa kanisa katoliki kote duniani, wengi ambao
wanashiriki katika kumchagua mrithi wake.
Makadinali hao wapya wanatoka
mabara matano akiwemo mjumbe wa Vatican nchini Syria.
Sasa Papa Francis amechagua
theluthi moja wa makadinali ambao watamchagua mrithi wake.
Ni makadinali walio chini ya
miaka 80 tu ambao wanaweza kumchagua Papa mpya. 13 kati ya wale walioteuliwa
wako chini ya miaka 80 na sasa wanahitimu kumrithi.
Ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka mitatu
ambapo Papa Franciss, ambaye ni Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini
kuwateua makadinali wapya
Makadilani hao wapya wanatoka
nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati , Bangladesh, Papua New Guinea na Mauriotius
miongoni mwa nchi zingine.
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment