Ni tamasha kubwa na la aina yake kuwahi kufanyika
jijini Mwanza,likiwa ni maalumu kwaajili ya kufunga mwaka kwa kumshukuru Mungu
kwa zawadi kubwa ya uhai.
Tamasha hilo la kusifu na kuabudu litafanyika
jumapili ya tarehe 4/12/2016 kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na mbili
jioni kwenye kanisa la TFE Kwaneema chini yake Bishop Augastine Mpemba lililopo
kona ya msumbiji Nyasaka jijini Mwanza.
Waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa
Mwanza watashiriki katika tamasha hilo akiwemo: Angel Benard kutoka,Moses
Butoi,Ajuwaye Onesmo,Janet John,Jerusalem Choir bila kuwasahau watoto wa
nyumbaji Kwaneema Band na wengine wengi.
Hakuna kiingilio katika tamasha hilo ni bure
kabisa,pia chakula cha mchana kitatolewa kwa wote watakaohudhulia.
Hii siyo ya kukosa,Wote Mnakaribishwa!
No comments:
Post a Comment