Karibu tuendelee na sehemu ya nne ya ushuhuda wa kweli wa mwimbaji Manonga classic.Ushuhuda unaitwa 'Mkasa wa Mama wa Kambo'.
AWALI YA YOTE NIWAOMBE RADHI SANA KWA WALE NILIOWAUMIZA MIOYO YENU SIKUJUA
KAMA ITAWAGUSA HII KITU HIVYO NAOMBA MNIWE RADHI NIIMALIZIE HII KITU.
BAADA YA KUWA NIMEPOTEZA FAHAMU KWA KILE NILICHOKIONA WAKATI WA USIKU ULE
NDIPO WENZANGU WALIPONIPITIA MAJIRA YA SAA KUMI KUELEKEA ALFAJILI WAKANIKUTA
NIKIWA NIMEZIMA KABISA NA NDIPO WALIPOANZA KUNIAMSHA BAADA YA MUDA NIKAWA
NIMEZINDUKA WALIPONIULIZA MBONA KAMA KUNA TATIZO LIMETOKEA NAMI SIKUWAELEZA
CHOCHOTE NILIRUDI NYUMBANI NIKIWA NA MASWALI MENGI MAMA YANGU ALINIPA POLE NDIO
UNAEMUONA HAPO KWA PICHA.
NILIACHA KAZI YA UVUVI WA USIKU NA KUANZA KUFANYA KAZI YA UVUVI WA HASUBUI
SAA MOJA HADI SAA NNE ASUBUI NILIENDELEA VYEMA NA KAZI HIYO SIKU MOJA NIKIWA
NIMEAMKA ASUBUHI NA KUKUSANYA VIFAA VYANGU VYA KAZI NIKACHUKUA MTUMBWI NA
KUELEKEA ZIWANI.NILIPOFIKA PEMBEZONI MWA ZIWA NILIUFUNGA MTUMBWI WANGU KWA
KAMBA KWENYE MTI ILI UWE KATIKA HALI YA UTULIVU NIENDELEE KUVUA.
WAKATI NIKIWA
NAENDELEA KUVUA KUMBE MAMBA MKUBWA ALIKUWA ENEO LILE NAMI PASIPOKUWA NA HABARI
NILIENDELEA KUVUA
GHAFLA NAFSI YANGU IKAJAWA NA HOFU NA WASIWASI MKUBWA NIKAWA KAMA NASIKIA
SAUTI PEMBENI YANGU IKINIAMBIA ONDOKA ENEO HILI SIKUJUA NIKWANINI KILA HATARI
ILIPOKUWA IKINIKARIBIA NAKUWA KAMA NASEMESHWA NA MTU NISIE MUONA.NILIPOANZA
KUFUNGUA KAMBA YA MTUMBWI NA KUANZA KUPIGA KASIA KUTOKA ENEO LA TUKIO GHAFLA
NILISIKIA KISHINDO KIKUBWA SANA KUMBE YULE MAMBA ALIKUWA AMETEGA CHINI YA
MTUMBWI WANGU ALITANDIKA MKIA WAKE KATIKA MTUMBWI WANGU ILI MTUMBWI WANGU
UYUMBE NIWEZE KUINGIA MAJINI NAMSHUKURU MUNGU NILIPATA UJASIRI WA KUUBARANSI
MTUMBWI WANGU GHAFLA UPEPO ULITOKEA NA KUNISAIDIA KUUPUSHI MTUMBWI WANGU NA
KUFANIKIWA KUTOKA KATIKA MAJI.
NILIAMUA KUACHANA NA KAZI ILE YA UVUVI NA KUFANYA KAZI ZINGINE ZA HAPA NA
PALE ILI MAISHA YAENDELEE MBELE.
SIKU ZIKAENDA MIAKA IKAENDA MAISHA YAKAWA BADO
NISHIDA NA TAABU NYINGI MUDA MREFU NIKAWA NIMEPOTEZANA NA YULE MAMA WA KAMBO NA
MAWAZO YAKE YOTE AKAWA ANAJUA TULISHAKUWA MACHOKOLAA WATOTO WA MITAANI NA
NDIVYO AKAWA ANAWASIMULIA RAFIKI ZAKE NA NDUGU ZAKE KUWA TULISHAKUWA WAMITAANI.
PALE NYUMBANI KWA MAMA MZAZI ALITOKEA DADA MMOJA ALIYENITAFUTIA KAZI KWENYE
KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA STATIONARY.
NAMSHUKURU MUNGU NILIZUNGUKA NA
ILE KAMPUNI TAKRIBANI MIKOA YOTE YA TANZANIA UTENDAJI WANGU WA KAZI ULIKUWA
NIMZURI NA BOSI ULIMVUTIA HATA KUFIKIA KUTOLEA MFANO KWA WAFANYA KAZI WENZANGU
KUMBE KITENDO KILE KILIWACHUKIZA SANA WENZANGU NA KUANZA KUWA WANANIFANYIA VISA
VINGI ILI BOSI ANICHUKIE.
WALIANZA KUFICHA VITU NA KUSEMA NIMEIBA WALIANZA
KUHARIBU VITU NA KUSEMA NI MIMI NDIPO BOSI ALIPOCHUKIA NA KUANZA KUNIPUNGUZIA
MSHAHARA WANGU KAMA ILIKUWA NALIPWA ELFU KUMI KWA SIKU BASI NALIPWA ELFU TANO.
HALI HIYO ILIZIDI NAKUFIKIA HATUA YA KUNIKATISHA TAMAA YA KUENDELEA NA KAZI
ILE.
NDIPO NILIPOAMUA KUACHANA NA ILE KAMPUNI NA KURUDI NYUMBANI KUANGALIA USAWA
MWINGINE.BAADA YA KURUDI NYUMBANI SIKU MOJA NILIJISIKIA NIENDE NIKAMSALIMIE
YULE MAMA WA KAMBO NIKIDHANI PENGINE LABDA ALISHAKUWA MTU MWEMA KUMBE
NILIVYOTARAJIA VILE HAIKUWA VILE SIKU YA KWANZA NILIENDA KUMUONA NA AKAWA KAMA
AMEPIGWA BUTWAA KUNIONA MAANA HAKUTARAJIA KAMA ANGEKUJA KUNIONA
TENA.NILIMSALIMIA NA AKANIITIKIA KINYONGE SANA NIKAMA HAKUFURAHISHWA NA UWEPO
WANGU MACHONI PAKE.
SIKU YA KWANZA ILIPITA KUMBE SIKUJUA YULE MAMA KAMA ALIKUWA
AMENIANDALIA MTEGO WA KUNIPOTEZA KABISA.
SIKU ILIYOFUATA NIKIWA NIMEENDA KUMSALIMIA RAFIKI YANGU PALE JIRANI NA
NYUMBANI ANAPOISHI YULE MAMA WA KAMBO NIKIWA NIMETULIA NDANI NAENDELEA NA
MAZUNGUMZO NA RAFIKI YANGU NDIPO MLANGONI IKASIKIKA IKIPIGWA HODI KUMBE NIMAASKARI
WAMETUMWA KUJA KUNIKAMATA KWA MARA YA KWANZA NAINGIA KWENYE MIKONO YA POLISI
PASIPOKUJUA KOSA LANGU NI NINI WALINICHUKUA NILIPOTAKA KUWAULIZA WALINIAMBIA
KUWA KUNA MAMA NILIMIPIGA NIKAWA NIMEMUUMIZA VIBAYA HIVYO NINAITWA NIKATOE
MAELEZO KITUONI.
NILIPOFIKA KITUONI NILISHANGAA KUMUONA YULE MAMA WA KAMBO AKIWA KITUONI NA
SURA YAKE IKIONEKANA KAMA YA MTU MWENYE GADHABU SANA NILIPOFIKA WAKANIULIZA
UNAMFAHAMU HUYU NIKAJIBU NDIO NAMFAHAMU ALIKUWA MKE WA BABA YANGU.
WAKASEMA
AMEKUSHITAKI KWA KOSA LA KUMTISHIA KUMUUA MIMI NILIKATAA NDIPO ALIPOULIZWA YEYE
KWAMBA UNAMSHITAKI AMA UNAMUONYA YEYE KWA HARAKA KABISA AKASEMA NINAMSHITAKI
PALE PALE NIKAVULIWA VIATU NA MKANDA NA VITU VYANGU VINGINE NILIVYOKUWA NAVYO
KABLA SIJATUPWA SERO NILIOMBA RUHUSA YA KUTOA TAARIFA KWA NDUGU ZANGU KUWA
NIMEKAMATWA NA NIKO KITUO CHA POLISI NA BAADA YA KUMALIZA KUTOA TAARIFA NDIPO
NILIPOTUPWA SERO HAPO NDIPO NILIPOIONA DUNIA CHUNGU NA NZITO NA MAISHA YA
MISUKOSUKO YAKAANZA UPYA FURAHA YA YULE MAMA IKATAWALA NA KUONA SASA
AMENIKOMESHA...
...HISTORIA YA MAISHA YANGU NITAKUJA KUIHITIMISHA KWENYE SEHEMU YA TANO NA
NDIPO UTAJUA NILIISHIA WAPI BAADA YA KUTUPWA SERO.
No comments:
Post a Comment