WAKRISTO WAZIDI KUUAWA NCHINI CUBA

 
Wakristo nchini Cuba pamoja na wachungaji wao wameendelea kupata mateso makali na makanisa yao kuchomwa moto sababu ni kutokana misimamo ya imani zao.

Kwa mujibu wa mtandao wa Christian Today wakristo hao wanapata mateso makali nchini humo pamoja na kwamba katiba ya nchi inakiri uhuru wa kuabudu kwa kila dhehebu.

Mchungaji wa Mario Felix Lionarti Barroso hivi karibuni alikaririwa  akisema kuwa damu za watu wengi katika nchi ya  Cuba zimemwagika kutokana na imani zao.

Aidha ameongeza kuwa pamoja na kwamba katika nchi katiba inaruhusu uhuru wa dini zote lakini bado wakristo wengi wanaendelea kuuwawa na kufanyiwa vitendo vya kikatili na serikali ya nchi hiyo kila kukicha.
 
Akitoa tathimini ya wakristo waliouawa alisema kuwa tangu January 2016 hadi Julai 2016 ndani ya nchi hiyo yamefanyika matukio 1,606 kwa wakristo ambapo ni pamoja na samani zake.

Alisema baadhi ya wakristo wengine wamekuwa wakiteketezwa ndani ya nyumba zao kwa moto na kuaribiwa mali zao bila kupata msaada wowote kutoka kwa serikali au jirani zao kwa kuhofia kuuawa. 


 

Chanzo:Gazeti la Jibu la Maisha
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment