Miaka michache baada ya kuzinduliwa kwa hekalu moja
la dini mseto kule Ujerumani linalojulikana kama CHRISLAM,likikusanya dini zote
chini ya paa moja,dunia imestaajabu tukio lingine muhimu kuelekea kutimia kwa
unabii wa Yohana(Ufunuo 13),baada ya wasomi wawili kuchapicha kitabu kimoja
kinachojumuisha vitabu 66 vinavyounda Biblia na aya zote zinazounda Quran
ili kuchukua nafasi ya Biblia na Quran zinazotumika kwa sasa.
Wasomi hao Safi Kaskas na Dk.David Hungerford
waliobobea katika tafsiri ya Quran na Biblia,wanadai kuwa kitabu hicho kinachokusanya
kwa pamoja maudhui ya Biblia na yale ya Quran,kitakuwa daraja muhimu kufikia
umoja wa kidini,utakaowafanya wanadamu kumwelewa Mungu vyema na hivyo kusali
pamoja bila kusigana kama ilivyo sasa.
Wawili hawa pia wanatajwa kuwa ni werevu katika
kutafsiri vitabu vya dini za Kiislamu na Kikristo,kwa kujibu maswali magumu yanayohusu
misimamo ya imani na pia ni wajumbe katika baraza la Kufikia Umoja wa Kidini
liitwalo Bridges to Common Ground.
Wanasema kuwa lengo lao kuu ni kuudhihirishia
ulimwengu kuwa kitabu cha mwongozo wa dini ya kiislamu Quran,hakiungi mkono
waumini wa dini hiyo kuua watu wa imani nyingine kwa jina la Mungu wao “Allah”lakini
kinawahimiza kutafta njia ya kuishi na wale wasio Waislamu kwa amani na umoja.
Wakinukuu Quran 5:48,wanasema kuwa kitabu hicho
kinaonesha kuwa Mungu aliumba makundi ya watu katika tofauti za kidini na
alitaka waishi hivyo na kama angetaka,angewaumba na utashi wa kuamini dini moja
tu.Wataalamu hao wanasisitiza kuwa zipo sura nyingi katika Biblia na Quran
zinazoeleza kwa pamoja kuwa Mungu ni wa huruma wakitoleaa mfano wa Zaburi 145:8
Kulingana na taarifa ya mtandao wa Christian Post,wasomi hao wawili wanatimiza unabii kwa
kulainisha misingi yenye kukinzana baina ya Uislamu na Ukristo na kuweka njia
sawa kufikia hatma ya dunia hii ya kuwa chini ya mtawala mmoja, dini moja na
serikali moja ya dunia na kwamba jukumu walilopewa wametimiza kwa mafanikio
makubwa.
Nani amewatuma kufanya kazi hiyo na wanafanya kwa
maslahi ya nani?Hayo ni maswali yaliyoibuliwa na wasomi wapinzani baada tu ya
kutolewa hadharani kwa kitabu kipya mbadala wa Qurani na Biblia zinazotumika
kwa sasa.
Profesa Leonardo Maniford mmoja wa wachambuzi wa
matukio ya mwenendo wa dunia,anaelezea kazi hiyo kama hatua ya juu kabisa ya
makundi ya waandaaji wa mfumo mpya wa dunia,wa kuingiza sayari hii katika
mkataba wa kumwabudu Lusifa(Shetani)kwa siri kubwa.
Inaelezwa kuwa kitabu hiki kinaandaliwa kama
mwongozo wa ukamilishwaji wa kazi ya ChriSlam,ili kuipitisha kwa siri katika
mabaraza ya makanisa na kupata msimamo mmoja kabla ya kukabidhiwa Umoja wa Mataifa
katika kile kinachoonekana kuwa ni kujenga umoja wa kweli wa kidini na
kufutilia mbali vitabu vyenye tafsiri inayounga mkono ugaidi.
Chanzo:Gazeti la Nyakati
0 maoni:
Post a Comment