![]() |
-Mhashamu Eusebius Nzigilwa |
Askofu
Msaidizi Wa Jimbo Kuu Katoliki Dar Es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa
Amekemea Waamini Wanaopenda Kufuatilia Vyombo Vya Habari Vya Kidunia Kuliko Vya
Kanisa Na Hivyo Kufanya Kazi Ya Uinjilishaji Kuwa Ngumu.
Hayo Yamesemwa Katika Misa Takatifu
Ya Kutoa Sakramenti Ya Kipaimara Katika Parokia Ya Teresia Wa Mtoto Yesu Mafia
Ambapo Takribani Vijana 30 Walipokea Sakaramenti Hiyo Idadi Ambayo Haijawahi
Kufikiwa Katika Kisiwa Hicho Cha Mafia Chenye Zaidi Ya Asilimia 90 Ya Wakazi
Wake Ni Waislamu.
Aidha Amesema Kuwa Yesu Amewaagiza
Watu Waende Ulimwenguni Kote Wakatangaze Injili Hivyo Hawapaswi Kupinga Agizo
La Mungu Na Kwamba Atakayemuonea Aibu Naye Atamuonea Aibu Mbele Ya Baba Yake.
Askofu Huyo Amewaasa Vijana
Waliopata Sakramenti Ya Kipaimara Kuwa Hata Wao Wanatumwa Kuitangaza Injili Na
Kuwataka Waitangaze Huruma Ya Mungu Bila Uwoga Kwani Huu Siyo Wakati Wa
Kujificha.
0 maoni:
Post a Comment