Kumekuwa na mtindo ambao unazidi kushika kasi wa waimbaji wa muziki kukopi aina flani ya miondoko kwa waimbaji walio mbali na wao(nje ya nchi)kisha kutumia miondoko hiyo ama kwa kuibadili kidogo au kuitumia kama ilivyo isipokuwa lugha tu ndiyo hubadilika.Tabia hiyo imekuwa ikishuhudiwa sana kwenye audios lakini sasa mambo yamebadilika hata kwenye videos wasanii wanacopy na kupast ideas na story za video.
Kwa mara kadhaa tabia hiyo imebainika na kuzusha maswali mengi kwa wadau na wafuatiliaji wa muziki juu ya uwezo wa waimbaji na pamoja na waongozaji wao wa video(directors),baadhi wanasema ni jambo la kawaida na la ubunifu huku wengine wakisema ni jambo la aibu na kukosa ubunifu.
Jambo hili limekuwa likishuhudiwa sana kwa waimbaji wa muziki wa kidunia lakini kumbe hata waimbaji wa muziki wa injili nao wanafanya tabia hiyo huenda hiyo inatokana na kushirikiana nao sana katika kufanya miziki pamoja,na mwishowe kujisahau na kujiona ni sawa na wao,anyway tusizame huko maana hiyo nayo ni mada nyingine tena pana sana.
Kwa mujibu wa kipindi cha mtandaoni kiitwacho BLUNDER kinachorushwa na mtandao wa YouTube channel ya NafiaAfrika,kimemtaja mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili kutoka chini Kenya William Paul maarufu kama Willy Paul Msafi kuwa amekopi hadithi ya video ya mwimbaji nguri wa nyimbo za kidunia kutoka nchini Marekani.Kupitia PROMOVER.COM tunakualika uweze kutazama ripoti hiyo katika kipindi hicho na kisha utoe maoni kuhusu tabia hiyo ili tuweze kufahamu mtazamo wako.
0 maoni:
Post a Comment