
Habari za kusikitisha kutoka China zinaeleza kuwa mtanzania mmoja Bi:Celina John aliyekamatwa kwa tuhuma za kuingiza dawa za kulevya nchini China mwishoni mwa mwaka jana akiwa sambamba na aliyekuwa mmewe mchungaji John Mangale ambaye alinyongwa katika tukio hilo,amejifungua watoto mapacha na sasa amepewa muda kidogo anyonyeshe kisha naye anyongwe na haijafahamika ikiwa watoto waliozaliwa gerezani watakuwa raia wa China na kulelewa na taifa hilo lenye imani kali za kuzuia uzazi atarejeshwa nchini.
Habari za uhakika kutoka kwa mtu wa karibu na
Celina zinasema kuwa,mama huyo aliyekamatwa na mmewe wakiwa pamoja na mtoto wa
miaka minne aliahirishiwa adhabu ya kunyongwa kwa kuwa alibainika kuwa alikuwa
mjamzito na akaamuliwa na serikali ya Uchina kuwa atasalia gerezani hadi
atakapojifungua na kupewa muda wa kunyonyesha kisha atanyongwa.
Nyakati linafahamu kuwa John aliwahi kuhudumu
katika kanisa la Breakthrough Assemblies of God lenye makao yake makuu Boko
jijini Dar es salaam,kwa muda lakini
miezi saba hivi kabla ya kutoweka aliaga kuwa anakwenda kufungua huduma yake
sehemu nyingine,hakuonekana kwa muda hadi pale taarifa zilipoibuka kuwa amekamatwa
na madawa hayo “unga” nchini China na kunyongwa.
Uchunguzi
wa Nyakati umebaini kuwa licha ya mchungaji aliyenyongwa kuwa na mtoto wa miaka
mine aliyesafiri naye pia ana binti mwingine(jina limehifadhiwa)ambaye yuko
darasa la saba na mtoto aliyekuwa na wazazi wake China tayari alirejeshwa
jijini Dar es salaam kwa msaada wa ubalozi wa Tanzania nchini China na
kukabidhiwa kwa jamaa zake.
Juhudi za kumpata mchungaji Gozbert Simtomvu
kuzungumzia habari za mama huyo aliyekuwa muumini wake kujifungua na kusubiri
kunyongwa hazikufanikiwa lakini wakati
mchungaji John aliponyongwa alinukuliwa na gazeti moja la kila wiki(sio
Nyakati)akikataa kuthibitisha kuhusu madai hayo,lakini alikiri kusikia taarifa
hizo ambazo ziliwaliza waumini wengi kwa vile mchungaji alikuwa mwanafamilia.

Chanzo: Gazeti la Nyakati
0 maoni:
Post a Comment