
WAKRISTO NCHINI WAMETAKIWA KUZIJUA KAZI ZAO NA
KUMTUMIKIA MUNGU KATIKA KIWANGO CHA JUU KWENYE IMANI ZAO ILI MUNGU AWEZE
KUIFUNGUA ARDHI NA KUKIKOMBOA KIZAZI KILICHOFUNGWA KATIKA MAAGANO YA MIZIMU NA
UKOO.
RAI HIYO IMETOLEWA NA ASKOFU MKUU WA KANISA LA HOLY
GHOST REVIVAL MINISTRY ILIYOPO IGOMA MITI YA NYERERE ASKOFU JOSEPHAT ROBART
MAGUMBA KATIKA SEMINA YA PASAKA ILIYOFANYIKA KANISANI HAPO.
AMESEMA ILI MUNGU AWEZE KUKOMBOA KIZAZI PAMOJA NA
ARDHI NI LAZIMA WAKRISTO WAWEZE KUMKIMBILIA MUNGU NA KUWEZA KUTUBU DHAMBI ZAO
KWA MAANA MUNGU HAKUMLAANI ADAMU BALI ALIILAANI ARDHI ILI ISIMKUBALI ADAMU .
PIA ASKOFU MAGUMBA ALIONGEZA KUWA DHAMBI UMFANYA
MWANADAMU KUONDOLEWA SURA YA MUNGU KATIKA MAISHA YA UKRISTO HIVYO NI LAZIMA
KILA MKRISTO KUJUA NAFASI YAKE NA KUSUDI LA MUNGU ILI LITIMIE KUWA WANADAMU
WAMEUMBWA KUWA WATAWALA TANGU MWANZO.
SEMINA HIYO ILIYOANZA TAREHE 12 APRIL 2017 NA ITAMALIZIKA 16 APRIL 2017.
0 maoni:
Post a Comment