EXTREEM AWARDS KE hizi ni tuzo kubwa kabisa za injili za nchini Kenya baada ya zile za Groove Award,na tuzo hizi zimeendeshwa kwa miaka mitatu sasa.
Katika tuzo hizo mwaka huu watanzania mbalimbali wameonekana
kuorodheshwa katika vipengele mbalimbali.
Moja kati ya waimbaji kutoka nchini Tanzania waliochaguliwa kushiriki tuzo hizo mwaka huu ni kikundi cha waimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza kinachoitwa KIHAYILE GROUP.
Kihayile group wameorodheshwa kwenye kipengele cha
Kimataifa-Afrika Mashariki –Wimbo wa Tanzania/Mwimbaji wa mwaka.Katika kipengele
hicho wanashindana na watanzania wengine Beatrice Kitauli na Krist kid kama
inavyoonekana hapo chini:
D. INTERNATIONAL CATEGORIES
DA TEENIZ EAST AFRICA - TANZANIA SONG / ARTIST OF THE YEAR 1 SIMON SIMONS
2 KRIST KID
3 BEATRICE KITAULI
4 KIHAYILE GROUP
Wakizungumza na PROMOVER.COM kiyahile wamesema ni jambo la kumshukuru mungu kwa hatua hiyo waliofikia na kwamba hiyo imetokana na juhudi zao binafsi kwa kuwa wamekuwa wakienda nchini Kenya karibia kila mwaka kwaajili ya kuhudumu lakini pia wamekuwa wakituma nyimbo zao nchini humo kupitia mitandao tu.
Aidha kihayile Grop wamewaomba watanzania kuwapigia kura ili waweze kuibuka katika kipengele hicho.
"Watupigie kura kwa wingi hata waimbaji wengine watuunge mkono ili dunia ijue Tanzania kuna vipaji vya muziki lakini pia italeta heshima si kwa kihayile tu bali kwa taifa lote na hata nje ya nchi,wajue Mwanza kuna waimbaji wazuri wanaomwimbia Mungu kwa roho na kweli”Amesema Abeid Kihayile
Christina Shusho |
Beatrice Kitauli |
Gudluck Gozbert |
Angel Benard |
Katika Tuzo hizo za mwaka huu watanzania wengine waliochaguliwa kushiriki ni pamoja na Christina Shusho kwenye kipengele cha Tuzo ya jumla kama inavyooneka hapa chini:
A. OVERALL CATEGORIES
AA TEENIZ AFRICAN ACTS
1 AA1 BAHATI - KENYA
2 AA2 CHRISTINA SHUSHO - TANZANIA
3 AA3 NATHANIAL BASSEY - NIGERIA
4 AA4 EXODUS - UGANDA
5 AA5 LEXKISS - MALAWI
6 AA6 COOPY BLY - UGANDA
7 AA7 VICKY NILAKAZI - SOUTH AFRICA
Mtanzania mwingine ni Gudluck Gozbert ambaye mwaka jana alitwaa tuzo hizo,mwaka huu yupo kwenye kipengele cha Wimbo wa Bongo/Mwimbaji wa mwaka kama inavyooneha hapa chini:
BE TEENIZ BONGO SONG / ARTIST OF THE YEAR
1 BE1 PERMINUS NDEGWA
2 BE2 EKASI MUSIQ
3 BE3 JOSE JAY
4 BE4 SILVER KENYA
5 BE5 BARNABUS MUINDI
6 BE6 ROY LWANGA
7 BE7 GOODLUCK GOZBERT
8 BE8 DAR MJOMBA
10 BE10 JULLY MWANAKOCHI
11 DF3 ROYALKID SIFA
Angel Benard pia ni mtanzania mwingine aliyeonekana kwenye kipengele cha Mwimbaji chipukizi wa kike kama inavyoonekana hapa chini:
AO TEENIZ NEW ARTIST (FEMALE)
1 AO1 ANGEL BENARD
2 AO2 BELLA D
3 AO3 SHINEL WANJA
4 AO4 SHARIMA BAHATI
5 AO5 CELESTINE DESTINED
6 AO6 HELIDAH OLUOCH
7 AO7 ROBBINAH JAY
8 AO8 PASTOR PAMELA OLOO
9 AO9 SHARON SHALLY
10 DE4 SHALATA
Mwaka jana 2015 Tanzania iliwakilishwa
na Goodluck Gozbert Enock Jonas, Bonny Mwaitege, Paschal Cassian na Edson
Mwasabwite na kati yao Goodluck Gozbert ndio aliweza kutwaa tuzo ya wimbo wa
mwaka.
Jinsi ya kuwapigia kura washiriki
uwapendao katika tuzo za mwaka huu,endelea kutembelea tovuti hii utapata
maelekezo ya kina.
JE! UNAPENDA SIMULIZI? BONYEZA>>HAPA
0 maoni:
Post a Comment