Wakristo wametakiwa
kupenda mafundisho ya neno la Mungu ili kuepukana na uzushi unao enezwa na
baadhi ya watu juu ya injili ili waweze kufika katika ufalme wa mbingu.
Hayo yamesemwa na askofu mkuu wa kanisa la Free Pendekoste Church of Tanzania(FPCT)Askofu David Batenzi,alipokuwa anazindua parishi mpya ya Mhonze mkoani Mwanza.
Amesema kuwa maombi na
mafundisho ni nguzo imara kwa mkristo ndiyo maana Yesu alifundisha watu kwa
njia ya maombi.
Askofu Batenzi pia amewaasa waumini wa parishi hiyo
mpya ya Mhonze kuweka watumishi walio jawa na roho mtakatifu ili kuweza kunena kwa lugha mpya na hivyo
kujenga mshikamano na umoja katika kumtumikia Mungu.
Kwa upande wake katibu
wa kanisa hilo Bw:Joakimu Makama
amepongeza sana uamzi huo wa
kuzindua kanisa hilo kuwa parishi mpya ambapo itakuwa na matawi ya Mhonze,Igalagala,Igombe,Kayenze
na Nyang’wilolelwa.
Aidha Bwana Makama
amesema uzinduzi wa kanisa hilo itawapatia wepesi wa kufanikisha kauli mbiu yao
inayosema kuwa ‘Leta mamilioni ya watu kwa Yesu’ kupitia mikutano ya injili na
ibaada ya nyumba kwa nyumba.
0 maoni:
Post a Comment