TANZIA:MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI NEEMA MWITA AFARIKI DUNIA

 

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza anayeitwa Neema Mwita,amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mbali na uimbaji pia Neema alikuwa ni mwandishi wa habari na mtangazaji ambapo amewawahi kufanyakazi kwenye vituo vya redio kadhaa za dini kama vile Kwaneema fm radio na HHC Alive fm.

Neema alitamba sana na wimbo wake unaoitwa "Watesi Wangu" ambao ulifanya vizuri na unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio nchini.Bila kusahau wimbo wake mwingine unaoitwa "Wanawake ni Jeshi kubwa"

Aidha Kabla ya mauti kumkuta Neema ailikuwa amejiunga na waimbaji wengine wa jijini Mwanza kusimamiwa shughuli zote za uimbaji na PROMOVER MANEGMENT ambao ndio wamiliki wa tovuti hii.

Uongozi wa PROMOVER.COM unapenda kutoa salamu za pole kwa familia ya Neema Mwita na wengine wote walioguswa na msiba huo.

Taarifa zaidi kuhusu Msiba huo na utaratibu wa mazishi tutazitoa kupita tovuti hii,endelea kutembelea

-download/Sikiliza hapa wimbo wake marehemu Neema Mwita unaoitwa Watesi Wangu
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment