Pengine tuseme uwezo wake unatokana na yeye kuzaliwa katika familia ya vipaji!ndio hilo linaweza kuwa jibu sahihi kwani Ibrahim amezaliwa kwenye familia ambayo wote ni waimbaji wa muziki kuanzia mama yake ambaye ni mwimbaji mkubwa tu na mkongwe kabisa wa nyimbo za injili anayeitwa Janeth Konje huku kaka zake Ibrahim nao wakiwa waimbaji wazuri tu.
Ibrahimu yuko darasa la 4 na maendeleo yake shuleni ni mazuri tu na anaweza kugawa vizuri muda wa masomo na sanaa.
Leo kupitia PROMOVER.COM Ibrahim anatualika tuweze kutazama wimbo wake mpya kabisa ambao umezinduliwa hivi karibuni huko wilayani Ukerewe wimbo unaitwa 'TUTARUKARUKA' ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kabisa japo kuwa anazo nyimbo nyingine nyingi tu kwa sasa.
Wimbo huo umerekodiwa kwenye studio ya Chile Records Chini yake Producer Chile Consumer na video imefanywa na Blue Ray Studio chini yake Director Mathayo.Karibu sasa uutazame wimbo huo.
Kwa mawasiliano zaidi ili kumpata mtoto Ibrahimu wasiliana na mamayake kupitia simu namba:0759 556 682 au 0789 028 655
-Download hapa audio ya wimbo huo wa Tutarukaruka -Kutazama picha za tukio zima la uzinduzi wa video hiyo,bonyeza>>HAPA
0 maoni:
Post a Comment