Katibu
Mkuu Wa Umoja Wa Madhehebu Ya Kikrsto Mkoa Wa Dodoma Askofu Dr Eliah Mauza
Amesema Kuwa Tanzania Imefungua Milango Ya Baraka Mbinguni Kwa Kuanzisha
Ushirikiano Na Taifa Teule La Israeli.
Askofu
Mauza Ameyasema Hayo Alipokuwa Akitoa Shukrani Zake Kwa Waumini Wa Madhehebu Ya
Kikristo Yaliyoshiriki Katika Maombi Maalumu Ya Mapatano Kati Ya Nchi Ya
Tanzania Ambayo Yalikuwa Na Lengo La Kufungua Milango Ya Kiroho,Kielimu,Na
Kiteknolojia Yaliyofanyika Mkoani Arusha Kwa Kushirikisha Nchi Zipatazo Tisa.
Amesema
Maombi Hayo Yamefanywa Na Kanisa La Tanzania Wakihudhuria Viongozi Wa Serikali
Yameonesha Uungwaji Mkono Wa Tanzania Kwa Taifa La Israeli Jambo Ambalo Ni Mwanzo Wa
Baraka Kwa Watanzania Hivyo Wanatakiwa Kuongeza Bidii Katika Kufanya Kazi Na Serikali
Kwa Uaminifu Huku Wakimtumikia Mungu Kiroho.
Kwa
Upande Wa Serikali Maombi Hayo Yaliwakilishwa Na Naibu Waziri Ofisi Ya Waziri
Mkuu Kazi Na Ajira Antony
Mavunde,Ambapo Nchi Zilizoshiriki Ni
Pamoja Na Amerika,AfrikaKusini,Nigeria,Kenya,Zambia,Burundi,Norway,Israel
Pamoja Na Tanzania.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Dk Susan
Kolimba (CCM),alisema hayo hivi karibuni bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Malindi,Ally Saleh Ally(CUF)lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Sikonge,Joseph
Kakunda (CCM).
Akijibu swali hilo,Dk Kolimba alisema Tanzania ilipopata Uhuru mwaka 1961,ilikuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Israel ambapo nchi hiyo ilikuwa na ubalozi wake jijini Dar es Salaam na Tanzania ilitumia ubalozi wake wa Cairo,Misri kuratibu uhusiano na Israel.
Alisema uhusiano huo uliingia dosari baada ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika(OAU)sasa Umoja wa Afrika(AU) kuitenga Israel.Hata hivyo,alisema kuanzia mwaka 1973 mpaka leo, kuna mabadiliko makubwa yametokea katika medani za kimataifa ikiwemo kumalizika kwa vitabaridi,kusambaratika kwa Muungano wa Jamhuri ya Kisoshalisti na Kisovieti.
Mambo mengine yaliyobadili medani za kimataifa ni pamoja na kuangushwa kwa Ukuta wa Berlin na kuungana kwa Ujerumani Mashariki na Magharibi pamoja na kupigwa hatua katika usuluhishi wa mgogoro wa Israel na Palestina.
Alitaja hatua hizo kuwa ni kutiwa saini kwa Mkataba wa Kwanza wa Oslo mwaka 1993,wa Pili mwaka 1995 na kuwepo kwa Mpango wa Amani wa Palestina.
Dk Kolimba alisema mwaka 1995,Tanzania ilichukua hatua ya kwenda na mabadiliko ya dunia na kuamua kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel,ambapo Israel ina Balozi wake Tanzania, mwenye makazi yake Nairobi,Kenya na Tanzania ina Balozi wake Israel,mwenye makazi yake Cairo,Misri.
Uhusiano huo kwa mujibu wa Dk Kolimba,umeendelea kukua hasa baada ya Tanzania kuwa na Sera mpya ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001,inayosisitiza diplomasia ya uchumi na kwa kutambua hatua kubwa iliyopiga na Israel katika kilimo, sayansi na teknolojia,Serikali imedhamiria kufungua ubalozi mpya Israel.
Pamoja na kufungua
ubalozi huo,alisema msimamo wa Tanzania katika kutetea haki za wanyonge
duniani,wakiwemo watu wa Palestina,bado uko palepale kama ulivyoachwa na
waasisi wa taifa.
0 maoni:
Post a Comment