HARUSI YA HONDWA MATHIASI YAZUA GUMZO MTANDAONI



Siku chache baada ya kutolewa rasmi wimbo wake Hondwa Mathias unaoitwa HARUSI,gumzo limezuka mitandaoni wengi wakionesha kufurahishwa sana na wimbo huo huku baadhi wakiwa wameshtushwa na wimbo huo.

Wanaoshtushwa na wimbo huo ni wale waliopokea taarifa hiyo kwa utofauti kabisa wakidhani kwamba mwimbaji Hondwa Ameoa.



Akihojiwa na kipindi cha burudani cha Full Shangwe Extra cha radio 98.2 kwaneema fm ya jijini Mwanza Nchini Tanzania,Hondwa amesema amepokea simu nyingi akiulizwa kwanini ameamua kufanya harusi kimya kimya bila kuwapa taarifa wadau wake.

Pia Hondwa anasema siku kadhaa tu baada ya kutoa wimbo huo tayari amepata mialiko zaidi ya 25 wakimtaka akatumbuize wimbo huo kwenye harusi zao.

Katika mahojiano hayo pia Hondwa ameeleza ni lini nayeye atafunga ndoa.Sikiliza mahojiano yote hapa chini kama alivyoojiwa na mtangazaji Peter Abdalah:

Kusikiliza wimbo huo wa HARUSI bonyeza>>HAPA

Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment