JENNIFER MGENDI KAAMUA KUWAFUNGUKIA ADUI ZAKE KWENYE WIMBO HUU MPYA

 
Mwimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Jennifer Mgendi ameuanza mwaka mpya wa 2017 kwa kuachia wimbo mpya wa audio unaoitwa 'Nawashukuru Adui'.

Wimbo huo unaopatikana kwenye album yake mpya inayoitwa 'Nyuma ya Mlima' umerekodiwa kwenye studio ya C9 Records chini ya mikono ya Producer C9.

Katika wimbo huo Jennifer anasema anawashukuru adui zake kwa kumfanya apige hatua za maendeleo kwani sio kila adui ni mbaya wengine wanatumiwa Mungu ili kuwafanikisha watu.

Jennifer anakualika uusikilize sasa wimbo huo kisha uusambaze kwa marafiki na maadui zako wote ukiwambia asanteni.Kwa mialiko,maoni na ushauri mtafte Jennifer kwa simu namba:0713 293 734 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment