BAADA YA MIAKA 200 HATIMAYE KANISA LA ANGLIKANA LAANZA KUTOA HUDUMA YA LITURUJIA



 
Kwa Mara Ya Kwanza Katika Historia,Imeelezwa Kuwa Kanisa La Anglikani Limeanza Kutoa Huduma Ya Liturujia Mjini Roma Miaka 200 Iliyopita. 
 
Ripoti Zinasema Kuwa Tangu Wakati Huo, Kumekuwepo Na Mabadiliko Makubwa Katika Mahusiano Kati Ya Kanisa Anglikani Na Kanisa Katoliki.

Aidha Hali Ya Kuwaziana Vibaya,Chuki Na Uhasama Kati Ya Waamini Wa Makanisa Haya Mawili Imepitwa Na Wakati,Kwa Neema Ya Mungu,Kwani Waamini Hawa  Sasa Wanaangaliana Kama Ndugu Katika Kristo.

Waamini Hawa Wanatambuana Kama Marafiki Na Mahujaji Wanaopaswa Kusafiri Pamoja, Ili Kumfuata Yesu  Kristo  Na Kuendelea Kuleta Umoja Na Mshikamano. 
 
Mshikamano Huo Unaonyesha  Upendo Wa Kristo Yesu Uliowagusa Waumini Wa Dini Zote Mbili  Kiasi Cha Kuamua Kuacha Yote Na Kumfuata Kristo.

Hapo Jana Papa Francis Kiongozi Mkuu Wa Kanisa Katoliki Duniani Katika Mahubiri Yake Wakati Wa Ibada Ya Pamoja Na Waamini Wa Kanisa Anglikani,Kama Sehemu Ya Maadhimisho Ya Jubilei Ya Miaka 200 Tangu Parokia Ya Wakatifu Wote,Amesema Kuwa Huruma Ya Mungu Ni Kiini Cha Utume Wa Kikristo Na Kwa Sababu Hiyo, Kamwe Hawapaswi Kulegeza Ushirikiano Huo.

Papa Fransic Amesema Hata Mtume Paulo Aliweza Kutekeleza Dhamana Hiyo Ya Umoja Na Mshikamano Kwa Njia Ya Unyenyekevu,Ambao Kimsingi Ni Fadhila Njema Kwa Watu Wote.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment