ALIYEFARIKI MIAKA 300 AFUMBUA MACHO MBELE YA WATALII.


Waswahili walisema dunia ina mambo na ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.huko nchini MEXICO kuna tukio la ajabu limetokea ambapo maiti ya mtoto iliyohifadhiwa kwa miaka 300 imeonekana ikifumbua macho.

Kufumbua macho kwa maiti huyo kulizua taharuki kwa ndugu na jamaa wa Santa Inocencia ambaye alikuwa mtoto wa kike ambayo imehifadhiwa katika sanduku iliyotengenezwa kwa kioo na watalii huruhusiwa kuitazama na hata kupiga picha.

Ni wakati wa mojawapo ya ziara hizo ambapo mtalii alikuwa akinasa matukio kwenye video, na kamera yake ilipofikia macho ya mwili huo, maiti ilionekana kana kwamba inafungua macho.

Video hiyo ilisambazwa mitandaoni na kuibua hisia tofauti huku baadhi wakisema ni ‘kiini macho’, huku wengine wakisema ni ishara ya mibaraka.

Inaaminika msichana huyo alikuwa raia wa Mexico aliyetaka kushiriki sacramenti yake ya kwanza na wanafunzi wenzake lakini akakatazwa na babake. Kulingana na hadithi kumhusu,alialikwa na watawa wa shule yake licha ya pingamizi la babake.

Babake alipopata taarifa alikiuka amri yake na kushiriki kwenye sacramenti, alimdunga kisu hadi akafariki.Inasemekana alihifadhiwa katika Kanisa Kuu la Kikatoliki eneo hilo kama ishara ya mapenzi ya dhati ya mtoto wa kike wa Kikristo.
Hilo limeelezwa kwamba ni tukio la kushangaza na la kwanza la aina yake kutokea nchini humo ambalo limetafsiriwa kama ni ishara ya baraka.Mpaka sasa hakuna taarifa kutoka serikalini inayoelezea tukio hilo la ajabu.

 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment