GOSPO AWARDS ni tuzo
maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na
wataarishaji wa muziki wa Injili walioweza kufanya vizuri kupitia tovuti
ya gospomedia.com mwaka 2016 kutoka
Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
Kwa mara ya kwanza tuzo
hizi zitatolewa tarehe 30.04.2017 jijini Dar es salaam.
SABABU ZA KUANZISHWA KWA
TUZO ZA GOSPO (GOSPO AWARDS)
1.
Kutambua na kuthamini kazi njema na jitihada za waimbaji na
wanamuziki wa nyimbo za Injili.
2.
Kutoa hamasa na ari kwa wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za
Injili.
3.
Kuleta mageuzi mapya katika tasnia ya muziki wa Injili Tanzania
na Afrika Mashariki kwa ujumla.
4.
Kuongeza chachu ya maendeleo ya ubora wa kazi za wanamuziki na
waimbaji wa nyimbo za Injili.
5.
Kupanua wigo wa soko la Muziki wa Injili kutoka ngazi ya kitaifa
kwenda kimataifa.
6.
Kutambua na kukuza vipaji vya waimbaji na wanamuziki wapya wa
nyimbo za Injili ili kuboresha tasnia ya muziki wa Injili.
7.
Kuhamasisha na kukuza ushirikiano na mshikamano baina ya
waimbaji, wanamuziki, na wadau mbalimbali katika tasnia ya muziki wa Injili.
Tuzo za GOSPO zitakuwa
zinafanyika mara moja kila mwaka ikishirikisha waimbaji, wanamuziki na wadau
mbalimbali kutoka kwenye taasisi, mashirika ya kiserikali, makampuni na watu
binafsi.
Vipengele vya Tuzo za
Gospo (GOSPO Awards) mwaka 2016/2017 zimegawanyika kama ifuatavyo
1.
Muimbaji bora wa kiume (Best Male Gospel Music Singer)
2.
Muimbaji bora wa Kike (Best Female Gospel Music Singer)
3.
Wimbo bora wa mwaka (Best Music Song of the Year)
4.
Video bora ya mwaka (Best video of the Year)
5.
Wimbo Bora wa kuabudu (Best Worship Song)
6.
Wimbo Bora wa Gospel HipHop (Best Gospel HipHop Song)
7.
Kundi/Bendi bora ya mwaka (Best Group/Music Band of the Year)
8.
Mtaarishaji bora wa Audio (Gospel Music Audio Producer)
9.
Mtaarishaji bora wa Video (Gospel Music Video Director)
10. Album
bora ya mwaka (Best Gospel Music Album)
11. Muimbaji
bora anayechipukia (Best Gospel Music Upcoming Artiste)
12. Wimbo
Bora wa kushirikiana (Best collabo)
13. Wimbo
bora wa mwaka kutoka Afrika mashariki (Best East African Song)
14. Mtangazaji
Bora wa Mwaka (Best Gospel Music presenter)
15. Kipindi
bora cha Radio (Best Gospel Music radio Program)
16. Kipindi
bora cha Tv (Best Gospel Music Tv Program)
17. Management/Label
bora ya mwaka
18. Achievement
Awards
19. Tuzo ya
heshima
20. Tuzo
Maalum (Special Award)
Baada ya sherehe za
utoaji wa Tuzo za gospo, uongozi na timu nzima ya gospomedia ikishirikiana na
wadhamini na wadau mbalimbali itajumuika pamoja katika kutoa shukrani kwa jamii
hasa kwa makundi maalumu kama vile watoto waishio kwenye mazingira magumu,
wagonjwa walio hospitalini, wazee waliokosa msaada na walemavu lengo la tukio
hili ni kufanya ibada ya pamoja katika kuwajali wengine walio katika hali ya
mahangaiko mengi na kuwakumbusha uwepo wa Mungu juu ya Maisha yao na kuwatia
Moyo.
Tuzo za
Gospo 2017 zinatarajiwa kutolewa tarehe 30 April 2017 katika ukumbi wa CCC
Upanga, Dar es salaam
Tanzania.
Kwa maelezo zaidi kuhusu tuzo za
Gospo wasiliana nasi kupitia WhatsApp: +255755038159 au piga simu namba
+255658293696 au tuandikie barua pepe gospoawards@gmail.com
0 maoni:
Post a Comment