-Mtoto Ivan |
Mtoto Ivan Philibart ambaye ni mlemavu wa viungo
karibia vyote mwilini amepata msaada wa baiskeli ya walemavu kutoka kwa taasisi
ya kijamii ya Faraja Mission Foundation(FAMIFO TANZANIA)wakishirikiana na wadau
mbalimbali.
Mtoto huyo mwenye miaka 14 anamatatizo ya uti wa
mgongo ambapo amekuwa akiishi ndani bila kutoka nje hiyo ikitokana na kipato
duni cha mama yake ambaye ni mzazi pekee anayemlea baada ya baba kukimba
familia.
Akizungumza na wandishi wa habari wakati wa kupokea
msaada huo Bi:Alkadi Kutaga ambaye ndiye mama Ivan amekishukuru kituo cha redio Kwaneema fm kwa kumfichua mtoto wake mlemavu na kupelekea kupata msaada kutoka
kwa wasamalia wema huku akitoa wito kwa wenye watoto walemavu kutowaficha ndani.
-Mama Ivan |
Kwa upande wake mkurugenzi wa taasisi ya kijamii ya
faraja mission foundation(FAMIFO TANZANIA)Bwn:Erasto Juma akizungumza wakati wa
kukabidhi msaada huo amewapongeza wadau mbalimbali kwa kufanikisha msaada huo
lakini pia akitoa wito kwa wananchi kuwasaidia wasiojiweza.
-Bwn: Erasto Juma |
Aidha mjumbe wa serikali ya mtaa ambaye pia ni kaimu
mwenyekiti wa mtaa wa kilimahewa A. kwa jina lingine mji mwema Bwn:Silidion Kabukiza amesema kwaneema fm radio pamoja na famiro wamefanya tukio la
kihistoria katika mtaa huo kwa kuweza kumfichua mtoto ivani huku akiwataka
wananchi kuendelea kujitokeza kumsaidia mtoto Ivan.
-Kutoka kushoto ni Mama Ivan,Ivan Pamoja naye Erasto Juma |
Kama hukupata nafasi ya kusikiliza Makala iliyorushwa na kituo cha redio cha Kwaneema Fm Radio inayomhusu mtoto Ivan,basi PROMOVERTZ.COM inakualika kuchukua nafasi hii kuisikiliza na kuitazama Makala hiyo.
0 maoni:
Post a Comment