Lile neo la
Bwana Yesu la “ikiwa wameutenda hivi mti mbichi itakuwaje kwa mti
mkavu”linatimizwa kwa kasi kwa wanaoungoja ufalme wa mbinguni katika maeneo
mbalimbali duniani.
Hii ni
pamoja na mateso ambyo maelfu ya wakristo yakiwemo mauaji ya kuteketezwa kwa
moto,kuchinjwa kama wananyama na kupigwa risasi,wanaendelea kuyapata.
Korea
kaskazini ni baadhi ya mataifa yanayodaiwa kuwa na rekodi kubwa ya kuhuskika
katika mateso hayo kwa wakristo nchini humo kwa muda mrefu sana,utafiti
umebaini.
Matokeo ya
utafiti yaliyotolewa na shirika linalohusika na masuala ya uhuru wa kidini
kutoka UK wiki iliyopita,inaonesha kuwa wakristo katika taifa hilo
wamekuwa katika mateso ya kiutumwa,kubakwa na kuuawa.
Kwa mujibu
wa mtandao wa habari za kikristo duniani ambao ulisambaza matokeo ya utafiti
huo,imani za kidini ukiwemo ukristo zimekuwa tishio kubwa kwa wakuu wa taifa
hilo na iwapo mtu yeyote atabainika kujihusisha nazo inampasa mateso makubwa.
Inaelezwa
kuwa wakristo wengi nchini humo wamekuwa katika mateso makubwa kutokana na
kutokuwa na radhi na utawala wa kibeberu na kupinga mapinduzi dhidi ya imani
yao.
Utafiti huo
umeendea kubainisha kuwa wakristo wamekuwa wakisurubiwa juu ya misalaba kwenye
moto,kukatwa vichwa,kuburutwa na kukanyagwa miguu.
Pia sera ya
nchin hiyo kuhusu ushirikishwaji,watu wote wenye undugu au urafiki na wakristo
wanatiwa hatiani kwa kupelekwa gerezani bila kujali wanauamini ukristo au laa.
“Hata raia wa Korea
kaskazini ambao wamekimbilia nchini China na ambao ni wakristo au wanakubali
kuwa wakristo wanarudishwa nchini kwao na kupelekwa kwenye makambi ya magereza
ya kisiasa” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hadi sasa
idadi ya wakristo nchini Korea Kaskazini kwa mujibu wa takwimu za Cornerstone Ministries International ni
kati ya 200,000 na 300,000 huku zile za kiserikali zikisema ni 13,000.
Hadi sasa
wakristo nchini humo wametakiwa kuendesha ibada kwa siri vinginevyo wasubiri
kwenda kwenye makambi ya mateso.
Wakati huo
huo,mamia ya wabunge,wanasheria chini ya
umoja wao wa IPPFoRB,wawawikilishi wa makanisa na wale wa mashirika yasiyo
ya kiserikali kutoka nchi mbalimbali duniani,wamejichimbia nchini Berlin Ujerumani
huku ajenda kubwa ikiwa ni kupinga mateso na unyanyasaji unaofanywa kwa
watu juu ya imani zao za kidini.
0 maoni:
Post a Comment