Mtoto wa kwanza aliyetengenezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa,jarida la kisayansi New Scientist limetangaza.
Wakikiuka
rasmi amri mpya aliyoitoa papa Francis hivi karibuni, wataalam wa tiba
wamefanikiwa kuingia maabara na kutengneza mtoto wa kiume mwenye chembe (DNA)kutoka
kwa mama yake,baba yake, pamoja na jeni za mfadhili.
Madaktari wa
marekani walichukua hatua hiyo kuhakikiha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru
kutokana na hali ya jeni ambayo mama yake kutoka Jordan anabeba katika mwili
wake.
Wataalam
wanasema kuwa,hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia
familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.
Lakini
wameonya kuwa, uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia
inayoitwa ‘Ufadhili wa Mitochondrial’unaitajika.
Mitochondrial
ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu
inayotumika mwilini.
Baadhi ya
wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na
wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.
Wanasayansi
waliohusika katika shughuli hiyo,walsafiri hadi Mexico kwa sababu huko hakuna
sheria za kuzuia shughuli kama hiyo ya kimatibabu.
Walichukua
sehemu muhimu za chembe za kinasaba (DNA)kutoka kwa yai la mama,na DNA ya
mitochondria kutoka kwa yai la mfadhili
na kuunda yai lenye afya ambalo lilitungishwa mbegu kutoka kwa baba.
Matokeo yake
ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye asilimia 0.1 ya DNA kutoka kwa mfadhili na jeni
nyingine zote,zinazoamua sifa kama vile rangi ya nywele na macho kutoka kwa
mama na baba.
Lakini
mchezo huo wa kisayansi tayari umekwaa kisiki kwa kuwa licha ya kanisa katoliki
kuupinga na kusababisha baadhi ya mataifa
ikiwemo marekani kuupiga marufuku, papa Francis ameamua kutengeza
amri mpya inayopiga marufuku uhandisi wa
jeni.
Kwa muda
mrefu, kanisa Katoliki lilipinga shughuli ya uhandisi jeni na ni kutokana na
nguvu zake,mataifa kadhaa duniani ikiwemo Marekani,yalipiga marufuku uhandisi
huo na hilo lilipelekea wanasansi wa Marekani kubeba wazazi watatu hadi nchi ya
Mexico na kufanyia shughuli hiyo huko Dk John Zhang,Mkurugenzi wa kimatibabu
katika hospitali ya New Hope Fertility Centre jijini New York City,amesema yeye
na wenzake walitumia njia hiyo kupata viineitete vitano lakini wakastawisha
kimoja tu.
Chanzo:Gazeti la Nyakati
0 maoni:
Post a Comment