MLEMBA MO AACHA GUMZO KIBONDO MKOANI KIGOMA



Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka jijini Mwanza Mlemba Moses maarufu kama Mlemba Mo, ameacha gumzo wilayani Kibongo Mkoani Kigoma,Baada ya nyimbo zake kukonga nyonyo za wananchi wengi waliojitokeza katika mkutano wa injili.


Mlemba Mo alihudumu katika mkutano wa injili wilayani humo hivi karibuni,ambapo mkutano huo ulikuwa maalumu kwaajili ya uzinduzi wa kanisa la The Great Restolation Ministry(TGRM).

 
Akizungumza na PROMOVER.COM Mlemba Mo alisema,alishangazwa na mapokezi mazuri ya wananchi wa Kibondo ambapo walifurahia sana na mara zote alipopanda jukwaaani hawakutaka ashuke kutokana na kuwagusa sana katika nyimbo zake.

 
Aidha Mlemba Mo aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo ya nyimbo Hasa nyimbo zake mbili za Nyamaza na Wale wale,ziliweza kuwavuta watu wengi katika mikutano hiyo ambapo wengi wao waliamua kumkabidhi Yesu maisha yao.

Tazama baadhi ya matukio katika picha mambo yalivyokuwa wilayani Kibondo.

 -Hawa ni baadhi ya wananchi waliohudhulia
 -Watumishi wa Mungu
 -Kazi Ya Mungu Ikiendelea
 -Mlemba Mo akitummbuiza

Kama hujawahi kupata nafasi ya kusikiliza nyimbo zake Mlemba Mo,nakuarika sasa uweze kusikiliza/kutazama moja kati ya wimbo wake uitwao 'Nyamaza'
 
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment