VYUO VIKUU VYA AFRIKA KUSINI KUANZA KUTOA DEGREE YA UCHAWI NA USHIRIKINA LENGO NI KUPUNGUZA JAM BARABARANI KWA WATU KUJIFUNZA KUPAA KWA UNGO



Kila kukicha dunia haiishi maajabu,mengine yakiwa ni yale ambayo yako kinyume kabisa na mapenzi ya mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na dunia.

Afrika kusini imeingia kwenye orodha ya ncchi za maajabu na vituko baada ya taarifa mpya za hivi karibuni kubainisha kuwa hivi karibuni vyuo vikuu nchini humo viitaanza kufundisha kisha kutunuku shahada(degree)ya masuala ya uchawi na ushirikina.

Waziri wa elimu ya juu na mafuzo wa nchini Afrika Kusini Blade Nzimande ametangaza mpango huo wa kuingiza masuala ya uchawi na ushirikina katika mtaala mpya wa masomo wa mwaka 2018 ili kuwapa nafasi ya kujifunza kwa undani masuala hayo wanafunzi ambao watakuwa tayari katika vyuo vikuu vya nchini humo. 

Waziri huyo ametangaza nia hiyo mbele ya wanafuzi katika mkutano wawakilishi wa umoja wa wanafunzi wa taifa hilo ambapo amesema lengo la kozi hiyo ni kuwapa ujuzi wa kutosha wanafunzi wanaovutiwa na masuala ya ushirikina kwa ustawi wa jamii.


“Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wachawi,kama vile jinsi wanavyopaa katika ungo.Hebu vuta picha kama tutajifunza ujuzi huo itamaliza kabisa tatizo la msongamano wa magari barabarani na kila mtu atapanda tu ungo na kupaa,inamaanisha pia kwamba hatutaingiza tena nchini mafuta ya magari”.Alisema Blade


Bwn:Blade aliongeza kuwa anatoa wito kwa wachawi wote wenye ujuzi kufika ofisini kwake ili wafanyiwe usahili na wale watakaopita waajiliwa kama walimu wa vyuo vikuu(lectures).


Aliongeza kuwa mwaliko huo pia unawahusu wachawi wote waliyoko nje ya Afrika kusini ambapo ameahidi kuwapa kibali cha kudumu cha wakazi.

“Nimeongea na Gibs(Waziri wa mambo ya ndani Malusi Gigaba)na amekubali kutoa vibali vya wakazi vya kudumu kwa wachawi wanaotoka nje ya Afrika kusini,naskia Malawi na Zimbabwe kuna wachawi wa viwango kibao,nimatumaini yetu wataitikia mwaliko” Aliongeza Blade 

  
Kutokana na tangazo hilo,wanafunzi wawakilishi katika mkutano huo walifadhahishwa na matamshi hayo kwani wengi wao walienda katika mkutano huo wakitegemea waziri huyo angetangaza ongezeko la 0% ya ada kwa mwaka ujao,ambapo katika hali ya kuoneshwa kuchukia walimzomea waziri huyo na kumponda kwa chupa za maji.


Maombi ya kujiunga na kozi ya uchawi na ushirikina kwa wanafunzi ambao wamevutiwa nayo inasemekana kufungwa September 30 usiku wa manane na  kutakuwa na nafasi za kazi kwa wachawi wapatao 109.

Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment