HII NDIO SABABU YA HONDWA MATHIAS KUADHIMIA KUSAIDI YATIMA NA WAJANE KUPIA TAMASHA LAKE JUMAPILI


Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Hondwa Mathiasi ameeleza sababu ya kwanini amekusudia kuwasaidia wajane na yatima kupitia pesa zitakazopatikana kama kiingilio katika tamasha la uzinduzi wa album yake utakaofanyika jumapili ya tarehe 20/11/2016.

Akihojiwa kwenye kipindi cha Full Shangwe Extra kinachorushwa na kitu cha redio ya kikristo cha jijini Mwanza 98.2 kwaneema fm radio,amesema kinachompelekea kukusudia kuwasaidia watoto yatima na wajane ni kutokana na shida nyingi alizopitia katika harakati zake za kutoka kimuziki.

Hondwa amesema mama yake mzazi alifikia hatua ya kuuza nyanya pamoja na biashara nyingine ndogondogo ili tu mwanaye apate hela ya kurekodi nyimbo.

Aidha Hondwa amesema hana masihala katika suala hilo na atahakikisha anawafikishia yatima na wajane msaada utakaopatikana kupitia sehemu ya mapato ya mlangano yatakayopatikana siku hiyo ya jumapili.

-Bonyeza play hapa chini kusikia maelezo zaidi kwenye mahojiano hayo:

-Kufahamu zaidi kuhusu tamasha hilo,bonyeza>>HAPA
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment