![]() |
Kushoto ni Moses Simkoko akiwa katika studio za Kwaneema fm radio |
Moses Simkoko kutoka Mbeya anasema alishangaa sana baada ya kuona wimbo wenye kufanana sana na wake na hiyo ilikuwa ni baada ya yeye kupost wimbo wake kwenye group la wasap ndipo mwanagroup mmoja akatuma wimbo mwingine unaofanana sana na wake ndipo zilipofanyika jitihada za kumtafta na kumuunga kwenye group hilo mwenye wimbo huo ambaye ni Christian Kelvin.
Mgogoro na bifu hiyo ilianzia rasmi hapo Baada ya Christian Kelvin mwimbaji maarufu kutoka jijini Mwanza kuwekwa kwenye group hilo ambapo Christian anadai alipokea matusi mengi sana inbox kutoka kwa moses baada ya wawili hao kupishana kauli.
Akihojiwa katika kipindi cha full shangwe extra kinachorushwa na kituo cha redio ya kikristo cha jijini Mwanza kinachoitwa Kwaneema fm radio,Simkoko amekiri ni kweli walipishana kauli na Christian hiyo ikitokana na mapokeo ya taarifa.
![]() |
Kushoto ni Moses Simkoko akiwa na Mtangazaji Erick Audax |
Bonyeza Play kusikiliza mahojiano hayo:
![]() |
Christian Kelvin |
![]() |
Moses Simkoko |
Sikiliza/download hapa nyimbo hizo mbili za waimbaji hao,zilizowapelekea kuhitilafiana kutokana na mashairi yake kufanana,na usiache kutoa maoni yako utwambie je! ni kweli nyimbo hizi zinafanana?
0 maoni:
Post a Comment