
KIONGOZI
wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Fransisko amemtunuku tuzo ya heshima
aliyekuwa mkuu wa Idara ya afya mstaafu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania
(TEC), Daktari Fredrick Kigadye kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwa kanisa
Katoliki.
Mwadhama,
Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, kwa niaba
ya Baba Mtakatifu Fransisko alikabidhi tuzo hiyo kwa daktari Kigadye jijini Dar
es Salaam katika hafla fupi iliyofanyika baraza la maaskofu.
Baada ya kukabidhi tuzo hiyo Kardinali Pengo alisema amejisikia furaha kwa tendo hilo kubwa katika kanisa lao hapa nchini la daktari Kigadye kupewa tuzo hiyo.
Baada ya kukabidhi tuzo hiyo Kardinali Pengo alisema amejisikia furaha kwa tendo hilo kubwa katika kanisa lao hapa nchini la daktari Kigadye kupewa tuzo hiyo.
“Daktari
Kigadye ametusaidia sana katika masuala ya Pasada kwa hiyo nina sababu ya ziada
ya yale yaliyoongelewa ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa tukio hili. Ni shukrani
kubwa kwa Baba Mtakatifu Fransisko aliyeridhia ombi la maaskofu kutoa hii hati
pamoja na nishani.Hati ikitolewa na Mwenyezi Mungu mambo mengine ni ziada,”
alisema Pengo.
Naye
daktari Kigadye alitoa shukrani zake kwa Mungu, Baba Mtakatifu Fransisko na kwa
maaskofu wote waliochangia jambo hilo kufanikiwa.
![]() |
-Daktari Fredrick Kigadye |
“Asante
kwa Mwenyezi Mungu kwa uhai na majaliwa yote kwangu na wote walioshiriki katika
malezi yangu hadi kufikia siku ya leo kihistoria,” alisema daktari Kigadye.
Kwa
upande wake rais wa Maaskofu Katoliki Tanzania, Tarcisius Ngalalekumtwa
alimtaka daktari huyo asijisifu wala kujivuna kwa kuwa jambo hilo lililofanyika
ni kazi ya Mungu.
Tuzo
hiyo ‘Bene Merenti’ maana yake ikiwa ni ‘kwa yule anayestahili’ ilipokelewa kwa
furaha na katibu mkuu wa TEC, Padri Raymond Saba.-Kutazama picha za hafla hiyo,>>Bonyeza HAPA
0 maoni:
Post a Comment