Wahitimu 2421 wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada, shahada za uzamili na uzamivu katika mahafali hayo huku wanafunzi wanafunzi 746 wakishindwa kutunukiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipia ada.
Mahafali hayo
yatatanguliwa na Siku ya Jamii itakayofanyika Jumatano Disemba 14 ambapo
kutakuwa na Maonesho ya Kitaaluma.
Wahitimu 2421
wa fani mbalimbali wanatarajiwa kutunukiwa vyeti, shahada,shahada za uzamili
na uzamivu katika mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine SAUT cha
Jijini Mwanza.
Makamu Mkuu wa
chuo hicho Dkt.Thadeus Mkamwa amesema wahitimu hao wakiwemo watatu wa shahada
za uzamivu watatunukiwa shahada zao kwenye Mahafali yatakayofanyika ijumaa na
jumamosi wiki hii chuoni hapo.
Amesema
mahafali hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la
Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Rwaichi yatatanguliwa na Siku ya Maonesho
Kitaaluma yatakayohusisha wanafunzi na wahadhiri kutoka kila kitivo na idara.
Hata hivyo
Dkt.Mkamwa amesema wanafunzi 746 wameshindwa kuhitimu masomo yao kutokana na
sababu mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa ada.(P.T)
Source: BMG Habari
Source: BMG Habari
0 maoni:
Post a Comment