RADI YALETA MAAFA MAKUBWA KWA FAMILIA YA MCHUNGAJI




Mtoto Wa Mchungaji Wa Kanisa La Evangelic Rukwa,Dorcas Andrew(5)Amefariki Baada Ya Radi Kumjeruhi Vibaya Kifuani Huku Mama Yake Mzazi,Rhoda Mlela (36) Akilazwa Kwa Matibabu Katika Kituo Cha Afya Kata Ya Sopa, Wilaya Ya Kalambo, Mkoani Rukwa Baada Ya Kupoteza Fahamu.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Rukwa,George Kyando Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Saa 11:00 Jioni Katika Kijiji Cha Sopa Kilichopo Katika Wilaya Ya Kalambo.

Mganga Mfawidhi Wa Kituo Hicho Cha Afya,Severine Maembe Amekiri Kumpokea Mtoto Huyo Kituoni Hapo  Lakini Mtoto Huyo Alikuwa Tayari Amepoteza maisha.
 
Ameongeza Kuwa Mama Mzazi Wa Mtoto Huyo Amelazwa Katika Kituo Hicho Kwa Matibabu Baada Ya Kupoteza Fahamu Muda Mfupi Baada Ya Kuelezwa Kuwa Binti Yake Amekufa Baada Ya Kupigwa Na Radi.

Baadhi Ya Mashuhuda Wanaeleza Kuwa Siku Ya Tukio Dorcas Na Mama Yake Walishuka Kwenye Gari Kijijini Hapo Wakitokea Mjini Sumbawanga Ambapo Mtoto Huyo Alipokewa Na Watoto Wa Rika Lake Na Kuanza Kucheza Pamoja Huku Mama Yake Mzazi Akielekea Nyumbani.
Share on Google Plus

About Promover

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment