WAIMBAJI MBALIMBALI WADIZI KUTHIBITISHA KUSHIRIKI KWENYE SEMINA KUBWA YA KUFUNGA MWAKA


Kuelekea ile semina kubwa kabisa kwa waimbaji ya kufunga na kufungua mwaka ambayo ni ya bure kabisa na itafanyika jijini Mwanza,waimbaji mbalimbali wameendelea kuthibitisha kushiriki.

Semina hiyo ni ya kwanza na ya kipekee kabisa kuwahi kutokea jijini Mwanza ikiwahusisha watangazaji wa vipindi vya injili(gospel)wa redio zote za mkoani humo.

Akizungumza na Promover.com katibu wa kamati ya maandalizi ya semina hiyo Bwn:Peter Abdallah kutoka kwaneema fm radio,amesema maandalizi ya semina hiyo yapo katika hatua nzuri ambapo pia waimbaji wengi sana kutoka ndani na nje ya Mwanza wameendelea kuthibitisha kushiriki.

Mwisho wa kuthibitisha ushiriki wako katika semina hiyo ni tar 28/12/2016 na namba ya kuthibitisha kwa kutuma Majina kamili tu ni 0755 255 844

Unatakiwa kutuma jina lako tu na utakuwa umethibitisha kushiriki katika semina hiyo ya bure itakayofanyika ijumaa ya tarehe 30/12/2016 kwenye ukumbi uliopo katika shule ya Kassa charity school kati ya igoma na kisesa kituo kinaitwa kanyama.

Semina hii inawahusu waimbaji wa nyimbo za injili na wale wanaotegemea kuwa waimbaji,ambapo watapata masomo mbalimbali ya kuwajenga na kuwapa mwongozo bora kutoka kwa watangazaji wa redio,waandaji wa miziki(producers)pamoja na wachungaji mbalimbali.

Kwenye semina hiyo pia waimbaji watapata fursa ya kueleza madukuduku yao kuhusu maendeleo ya muziki wa injili ikiwa ni sambamba na kutoa maoni ya kina juu ya kuujenga muziki huo na waimbaji wake.

Hii siyo ya kukosa,ukipata taarifa hii tafadhali mwambie na mwenzio wote mnakaribishwa.Semina hii imeandaliwa na Umoja wa watangazaji wa vipindi vya gospel jijini Mwanza wakishirikiana na Promover Manegement
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment