HII HAPA VIDEO YAKE MESS JACOB CHENGULA ILIYOGHARIMU TSH.MILLION 7




Kabla mwaka 2016 haujafika tamati,mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania anayeitwa Mess Jacob Chengula aliachia video ya wimbo wake wa 'USILIE' video ambayo kwa sasa imezua gumzo sana mtandaoni.

Gumzo kuhusu wimbo huo ni kutokana na gharama za utengenezaji wa video hiyo zilizotajwa naye Changula wakati akihojiwa kwenye moja ya vituo vya Televisheni ya nchini Tanzania.

Chengula alisema gharama ya video ya wimbo huo aliomshirikisha Emmanuel Mgogo iliyoongozwa na Director Einxer ni Tsh Milioni saba.

Gumzo mtandaoni linatokana na ukweli kwamba waimbaji wengi wa nyimbo za injili nchini Tanzania wamezoea kutoa video za bei nafuu sana ambazo zimekuwa hazina ubora mzuri,hivyo wengi wakishangazwa na bajeti ya video hiyo.

Yote kwa yote ni kwamba video hiyo ambayo kwa uhalisia nikweli ina ubora wake,ipo hadharani kwa sasa na leo kupitia Promover.com Chengula anakualika uitazame kisha kama una maoni usisite kucomment hapo chini.Ubarikiwe sana!

Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment