HIVI NDIVYO KANISA LA TFE KWANEEMA LILIVYOUKARIBISHA MWAKA 2017


Jumamosi ya tar 31/12/2016 ndo ilikuwa siku ya mkesha kwaajili ya kuupokea mwaka mpya wa 2017 ambapo katika kanisa la TFE kwaneema mkesha huo ulfana sana kwani wakazi wengi wa jiji la Mwanza walijitokeza kupokea Baraka za Mwaka mpya.

Mkesha huo ulioongozwa na mchungaji kiogozi wa kanisa la TFE Kwaneema Mch Philipo Stanslaus kwa ushirikiano na Mchungaji Paul Chaba.

Wakristo Nchini Wametakiwa Kujichunguza Na Kujiuliza Maswali Mawili Katika Maisha Yao Pindi Mungu Akiwachukua Na Kuwauliza Walifanya Nini Duniani Juu Ya Yesu Na Pia Walifanya Nini Juu Ya Kutumia Karama Zao Katika Kumtumikia Mungu Na Maisha Yao Kwa Ujumla.

Kauli Hiyo Ilitolewa Na Askofu Mkuu Wa Kanisa La Tanzania Field Evangelism T.F.E Kwaneema Askofu Augastine Mpemba Katika Mkesha Wa Kufunga Mwaka 2016 Na Kuupokea Mwaka 2017 Katika Kanisa La T.F.E Kwaneema Lililopo Kona Ya Msumbiji Jijini Mwanza.
Alisema Katika Maisha Ya Ukristo Ni Lazima Kila Mkristo Ajue Kuwa Kuna Siku Ambayo Utasimama Mbele Za Mungu Na Kuweza Kumwambia Habari Zako Jinsi Ambavyo Uliishi Katika Dunia Hii Na Pindi Ushindwapo Kujibu Maswali Ya Mungu Utapokea Matokeo Ya Majibu Yako.


Pia Skofu Mpemba Alingeza Kuwa Katika Mwaka 2017 Ni Mwaka Wa Kukaza Mwendo Haijalishi Hata Kama Kuna Magumu Mangapi Ambayo Watu Wanapita Ila Ni Mwaka Wa Kukaza Mwendo Kwa Ajili Ya Kufanikiwa Zaidi.


Kutazama picha zaidi,Bonyeza >> HAPA
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment