KIHAYILE GROUP KUACHIA VIDEO YA MTENDA MIUJIZA HIVI KARIBUNI



Kikundi cha waimbaji wa nyimbo za injili cha Kihayile Group cha jijini Mwanza,kinategemea kuachia video ya wimbo wao wa Mtenda Miujiza hivi karibuni.

Wakizingumza na Promover.com Kihayile Group ambao mwishoni mwa mwaka 2016 walitwaa tuzo za njili huko nchini Kenya wamesema punde tu baada ya tuzo hizo walijichimbia location kwajili ya kutengeneza video za nyimbo zao mbalimbali ambazo watakuwa wakiziachia moja baada ya nyingine.

Kihayile Group wamewataka wadau wa muziki wa injili kukaa tayari kwaajili ya video hiyo ya Mtenda Miujiza ambayo iko katika viwango vya kimataifa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment