MANONGA CLASSIC KAACHIA YAKE YA KWANZA KWA 2017 | USISHINDANE




Kwa mara ya kwanza kabisa kupitia tovuti yako namba moja ya masuala ya Gospel Promover.com leo utapata fursa ya kuusikia wimbo mpya kabisa kwa mwaka 2017 wake Manonga Classic wimbo unaofahamika kwa jina la 'USISHINDANE'.

Baada ya kungoja kwa siku kadhaa hatimaye Manonga ameichagua siku ya leo kuwa siku maalumu kwaajili ya kuuachia wimbo huo unaotoa onyo kushindana na mtu aliyebarikiwa ukiwa umerekodiwa kwenye studio ya MP Record ya jijini Mwanza Producer akiwa ni Ibrahim Mwasposya.

“Unajua unapoianza safari wanadamu wanakutia moyo sana lakini mafanikio yanapoanza kuonekana wanaanza kuinua vikwazo juu ya Baraka zako na kuanza kupambana ili wakushushe,lakini mpango wa Mungu ukishatimia kwa Mwanadamu hayupo wa kuuharibu hivyo huwezi kushindana na mtu aliyebarikiwa”.Amesema Manonga.

Pia Manonga ameongeza kuwa “Ukitaka kumshusha mtu aliyeinuliwa nenda kwanza ukazungumze na Mungu mwenyewe aliyemuinua na kumbariki akikubali hapo utakuwa umefanikiwa vinginevyo Huwezi kushindana na mtu aliyebarikiwa na Mungu”.

Manonga amewataka wadau wake wote kuupokea wimbo huo kwa mikono miwili,wausambaze kwa marafiki kisha kutoa maoni.Kwa mawasiliano ili kumpata Manonga piga simu namba:0752 690 120
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment