MANONGA CLASSIC KUACHIA WIMBO MPYA | USISHINDANE NA MBARIKIWA


Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili kutoka jijini Mwanza Manonga Classic,anatarajia kuachia wimbo mpya wa audio ambao ndio utafungua mwaka mpya wa 2017.

Akizungumza na Promover.com Manonga amesema wimbo huo atakaouachia hivi karibuni unaitwa 'USISHINDANE' na mtu aliyebarikiwa.

“Unajua unapoianza safari wanadamu wanakutia moyo sana lakini mafanikio yanapoanza kuonekana wanaanza kuinua vikwazo juu ya Baraka zako na kuanza kupambana ili wakushushe,lakini mpango wa Mungu ukishatimia kwa Mwanadamu hayupo wa kuuharibu hivyo huwezi kushindana na mtu aliyebarikiwa”.Amesema Manonga.

Pia Manonga ameongeza kuwa “Ukitaka kumshusha mtu aliyeinuliwa nenda kwanza ukazungumze na Mungu mwenyewe aliyemuinua na kumbariki akikubali hapo utakuwa umefanikiwa vinginevyo Huwezi kushindana na mtu aliyebarikiwa na Mungu”.

Manonga Classic amewataka wadau wake kukaa tayari kwaajili ya kuupokea wimbo huo uliojaa Baraka na matumaini tele.Ili kumpata Manonga kwaajili ya mialiko,maoni na ushauri,mtafte kwenye simu namba:0752 690 120 
Share on Google Plus

About Jacktan Msafiri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment